MAJERAHA YA FIMBO KAMA YANAVYOONEKANA 

 Dada Mesoni Kashiro (15) mkazi wa kijiji cha Gelailumbwa kata ya Gelailumbwa wilaya  Longido Mkoani Arusha, ameshambuliwa na mume wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.


Unaambiwa walimfunga kwenye mti wakaanza kumcharaza viboko.

Taasisi za kuzuia ukatili wa ndoa za utotoni na mateso ya utumwa zimeombwa kufuatilia hili jambo na haki itendeke kwa mtoto huyu kwanza kwa kuolewa akiwa mdogo pili kukosa haki yake ya malezi na makuzi kama mtoto na tatu kwa kupigwa kipigo kikali kisicholingana na umri wake