WMA MAKAO YATOA COMPUTER 11 NA PRINTER 11 KWA SHULE 11 ZILIZO KATIKA VIJIJI VINAVYOUNDA JUMUIYA HIYO.


Na Berensi china Meatu.

Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori makao iliyopo wilayani meatu mkoani Simiyu imetoa msaada wa vifaa vya tehama kwa shule 11 za msingi zilizoko katika vijiji vinavyounda jumuiya hiyo.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni printer 11 na computer mpakato 11 aina ya dell vyote vikiwa na thamani ya shilingi milion 17.6.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa waalimu hao mkurugenzi wa halimashauri hiyo .Newaho mkisi ameipongeza jumuiya hiyo kwa msaada huo ambao.utawasaidia waalimu kuendana na mitaala mipya.


"Nawapongeza sana kwa uamuzi huo wa kusaidia hizi shule  nina imani wahusika watavitunza vifaa hivi ili viweze kuwasaidia katika shughuli zao"amesema mkurugenzi huyo


Kwa upande wake mkiti wa jumuiya hiyo  Danie Sengeka  amesema msaada ni sehemu ya mwendelezo wa jumuiya hiyo wa kusaidia wa.kusaidia vijiji huyo ambapo ameeleza matumaini yake kwa shule hizo kuwa vitaleta mabadiriko kwa kuwarahisishia waalimu katika utendaji kazi wao


Akitoa shukrani kwa niaba ya waalimu.wakuu waliokabidhiwa msaada huo mkuu wa shule ya msingi iramba ndogo.mwalimu saumu Ramadhani amesema wamepokea msaada huo kwa furaha kubwa ambapo amesema watahakikisha wanavitunza vifaa hivyo ambapo ameipongeza jumuiya hiyo kwa kuwasaidia kwani wamekuwa na changamoto hiyo kwa muda mrefu.

Hafla ya kukabidhiwa vifaa  hivyo imefanyika katika ofisi ya mkurugenzi wa halimashauli ya wilaya hiyo na kuhudhudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa baraza la jumuiya hiyo na maafisa kutoka idara ya elimu.

Mwisho