LEONARD BUGOMOLA
MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA GEITA
Baraza la Madiwani la Manispaa ya Geita limepitisha kwa kauli moja azimio la kusitisha mkataba wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) kati ya Manispaa hiyo na Mgodi wa GGML katika miradi miwili ukiwemo ujenzi wa uwanja wa mpira wa Magogo.
Na kwanza tamko rasmi la kusitisha mkataba baina ya GGML na Halmashauri likasomwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Geita Elias Ngole……
Uamuzi huo umehusisha miradi mikubwa miwili iliyokuwa ikitekelezwa kwa ushirikiano na mgodi huo, ambayo ni ujenzi wa soko la dhahabu pamoja na uwanja wa mpira wa Magogo.
ENG CHACHA WAMBURA
MBUNGE WA JIMBO LA GEITA MJINI
Madiwani wameeleza kusikitishwa na kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo, hali ambayo imewafanya kufikia uamuzi wa kusitisha mkataba huo.
Katika sakata hilo, suala la ujenzi wa Uwanja mpira wa Magogo limeonekana kuwa miongoni mwa ajenda muhimu, kutokana na wapenzi wa soka kuendelea kuhoji maendeleo ya ujenzi huo.
ELIAS NGOLE
NAIBU MEYA MANISPAA YA GEITA
Meya wa Manispaa ya Geita Leonard Bugomola amesema kama Manispaa hawataki fedha bali walitaka kuona matokeo chanya kwenye mradi wa uwanja.
Na hapa Mkurugenzi wa Manispaa ya Geita Yefred Myenzi anapokea azimio hilo kwa autekelezaji.






0 Maoni