Na Rose Mweko, Geita.
Wananchi wa Jimbo la Busanda, wamepongeza hatua ya Rais Samia Hassan kumteua Mbunge wao Dr.Jafari RAJABU Seif kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia Afya.
Wakizungumza nyakati tofauti wamesema ni heshima ya kipekee ambayo haijawahi kutokea tangu jimbo hilo kuanzishwa Ambapo umeleta faraja na matumaini mapya kwao huku wakieleza kuwa kwa mara ya kwanza Busanda imepata mwakilishi wa ngazi ya Uwaziri serikalini.
Wameeleza kuwa uteuzi huo unathibitisha dhamira ya Rais Samia kuhakikisha maeneo yote yanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo ya taifa hasa hasa kundi la vijana.
Wamesema wanaamini kuwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutoka Geita - kahamaa utafungua fursa za kiuchumi na kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.
Katika Sekta ya afya wameiomba serikali kupitia Dkt. JAFARI kuboresha vituo vya afya na zahanati kwa kuongeza dawa, vifaa tiba na huduma za uhakika muda wote ili kupunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji matibabu.






0 Maoni