MGOMBEA UDIWANI KATA YA BUKOLI FARAJI RAJABU SEIF 

Mgombea udiwani wa Kata ya Bukoli, Faraji Rajabu Seif, amemshauri mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda ambaye pia ni mdogo wake, Dkt Jafari Rajabu Seif , kuhakikisha anazingatia changamoto za wananchi iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge.

Akizungumza katika  uzinduzi wa kampeni  ya udiwani kata ya Bukoli uliofanyika Bugogo Senta, Faraji alimhimiza Jafari kuwa kiongozi wa karibu na wananchi na asiwe mbunge wa kukaa mjini Dodoma tu bila kushughulikia matatizo ya wananchi waliomchagua.

“Wananchi hawa unaowaona wanahitaji kuwa karibu na wewe, hivyo jitahidi katika uongozi wako uwe karibu na wananchi wako,” alisema Faraji.

Aidha, Faraji alisisitiza kuwa wananchi wa Jimbo la Busanda wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji kiongozi makini na mwenye kujitolea kuwa karibu na jamii ili kuzitatua.