DKT JAFARY RAJABU SEIF,MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUSANDA.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jafari Rajabu Seif, amemuomba mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuanzisha halmashauri mpya kwa ajili ya maeneo ya Katoro na Busanda baada ya  kuchaguliwa  katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.



Dkt. Jafari alitoa ombi hilo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita, akisema kuwa kuanzishwa kwa halmashauri hiyo kutapunguza adha kwa wananchi wa Busanda ambao kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za halmashauri katika eneo la Nzera.

"Mambo aliyoyafanya Dkt. Samia katika Jimbo la Busanda ndani ya miaka minne ni makubwa na yanayogusa maisha ya wananchi Hata hivyo, tunaomba pia jambo hili la halmashauri mpya liangaliwe ili kuwasaidia zaidi wananchi wetu," alisema Dkt. Jafari.

Mbali na hilo, Dkt. Jafari pia aliomba Serikali ijayo iangalie uwezekano wa kujenga barabara ya lami  ya Geita- kakola  katika jimbo hilo, akisema ni hitaji muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wakazi wa Busanda.