Baadhi ya wananchi kata ya Matendo Jimbo la Kigoma kaskazini wakisikiliza ujumbe kutoka uwt
Kigoma
Katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kushika hatamu za uongozi katika ngazi zote, Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kigoma umefanya kampeni za ndani katika Kata ya Matendo kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuendelea kuiamini CCM na kuwaombea kura wagombea wake katika uchaguzi ujao.
Bisura Mboge Mwk UWT (W) Kigoma vijijiniKampeni hizo zimeongozwa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kigoma vijiii Bisura Mboge,Mratibu wa UWT Mkoa wa Kigoma, Bi. Rose Mweko na madiwani vitimaalum ambapo wamesisitiza umuhimu wa wanawake na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi, huku wakijielekeza kuwachagua viongozi waadilifu na wenye dira ya maendeleo.
Katika kampeni hizo, UWT iliwataka wananchi wa Kata ya Matendo kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuwaletea Watanzania maendeleo, hasa katika nyanja za afya, elimu, miundombinu, na uwezeshaji wa wanawake.
Vilevile, waliwaomba wananchi kumpigia kura Peter Serukamba, mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, wakimtaja kuwa ni kiongozi makini, mwenye uzoefu na maono ya kuendeleza Wilaya ya Kigoma.
William Ndikumwami mgombea udiwani kata ya matendoAidha, walimnadi pia William Ndikumwami, mgombea udiwani wa kata hiyo, kama kiongozi mwenye ukaribu na wananchi na mwenye rekodi nzuri ya utendaji kazi.
Bi. Rose Mweko aliwahimiza wanawake kushikamana na kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha CCM inaibuka na ushindi mnono, huku akisisitiza kuwa kampeni hizo za ndani ni muhimu katika kujenga mshikamano, kusikiliza maoni ya wananchi, na kuwaelimisha kuhusu sera na mipango ya chama.
Bi Rose MwekoKampeni hizo ziliambatana na mikutano ya hadhara, uhamasishaji wa nyumba kwa nyumba, na usambazaji wa vifaa vya chama, huku wakitoa elimu kuhusu umuhimu wa amani, mshikamano na ushiriki wa wanawake katika siasa.
UWT Kigoma imeahidi kuendelea na kampeni katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa CCM kuanzia ngazi ya Rais, Mbunge hadi Diwani.
0 Maoni