MKUU WA MKOA WA GEITA MARTINE SHIGELLA 

NA ROSE MWEKO, GEITA.

Wananchi wa Mkoa wa Geita wameombwa kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru utakaopokelewa Septemba 1, 2025, katika Kijiji cha Rwezera, Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ukitokea jijini Mwanza.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, amesema Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu utakagua jumla ya miradi 61 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 164  ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka jana ambapo miradi 65 yenye thamani ya takriban shilingi bilioni 32 ilikaguliwa.


"Mwaka huu Mwenge utakagua miradi mikubwa yenye thamani ya zaidi ya bilioni 164. Hii ni ishara kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kufanya kazi kubwa ya maendeleo katika Mkoa wa Geita," alisema Shigela.


Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru na kushiriki katika shughuli mbalimbali zitakazofanyika.


"Nawaomba wananchi wa Geita tujitenge muda na kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru pale Rwezera," aliongeza.