Dkt. Jafary Rajabu Seif Ateuliwa na INEC Kugombea Ubunge wa Jimbo la Busanda
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imemuidhinisha rasmi Dkt. Jafary Rajabu Seif kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Busanda katika uchaguzi mkuu ujao. Uteuzi huo umetangazwa na Sarah Yohana msimamizi wa INEC Halmashauri ya wilaya ya Geita baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchambuzi na uhakiki wa wagombea waliowasilisha nia ya kuwania nafasi hiyo muhimu ya uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na INEC, Dkt. Seif ametimiza vigezo vyote vinavyotakiwa kisheria na kikatiba, vikiwemo vya kielimu, kimaadili, na uwasilishaji sahihi wa nyaraka zote zinazohitajika. Tume imeeleza kuwa uteuzi wake unazingatia pia sifa zake za uongozi na mchango wake katika maendeleo ya kijamii na kisekta.
Dkt. Jafary Rajabu Seif ni mtaalamu wa Afya mwenye uzoefu mpana katika nyanja za kijamii na kiuchumi, na anajulikana kwa ushawishi wake mkubwa katika masuala ya maendeleo ya jamii. Wananchi wa Jimbo la Busanda wamepokea taarifa za uteuzi wake kwa hisia mseto, huku wengi wakionesha matumaini kuwa ataweza kuleta mabadiliko chanya endapo atapata ridhaa ya kuwatumikia kama Mbunge wao.
Katika mahojiano mafupi baada ya uteuzi huo, Dkt. Seif ameahidi kufanya kampeni za kistaarabu, zenye kuzingatia hoja na masuala ya msingi yanayowakabili wakazi wa Busanda. Pia ametoa wito kwa wafuasi wake kushiriki mchakato wa uchaguzi kwa amani na utulivu, huku akisisitiza umuhimu wa kuheshimu maamuzi ya wananchi.
Mpaka kufikia saa 10:00 jioni jimbo la Busanda lilikua na mgombea mmoja kutoka Chama cha Mapinduzi ambaye ni Dkt Jafary Rajabu Seif
kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi, na kuzingatia maadili ya kisiasa wakati wote wa kampeni na baada ya uchaguzi.
Kwa sasa, macho na masikio ya wananchi wa Busanda, pamoja na taifa kwa ujumla, yanaelekezwa kwenye harakati za kampeni kuelekea siku ya kupiga kura, ambapo watapata fursa ya kuchagua kiongozi watakayemwamini kuwa sauti yao katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Maoni