MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Geita mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhandisi Chacha Wambura amefika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi kuchukua fomu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ili kugombea nafasi hiyo.
Mhandisi Chacha amechukua fomu hiyo Agosti 25, 2025 na kueleza kuwa ajenda kuu kuelekea kampeni za uchaguzi mkuu ni 'Kazi na Matokeo' ambayo itasaidia kufanikisha ajenda ya CCM Taifa ya Kazi na Utu.
Amesema kupitia 'Kazi na Matokeo' anaamini akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Geita mjini atasukuma utendaji wenye kuleta matokeo yenye tija kwa jimbo hilo ambalo kwa sasa ni halmashauri ya Manispaa.
Amesema yupo tayari kushirikiana na ofisi ya mbunge aliyepita ili tu kuwezesha ukamilishaji wa maono yaliyokuwepo na hata kuanzisha maono mapya kwa dhumuni la kuijenga Geita yenye maendeleo zaidi.
0 Maoni