DKT.JAFARI ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUSANDA
DKT JAFARY RAJAB SEIF AKICHUKUA FOMU OFISI ZA HALMASHAURI US GEITA
Mgombea ubunge wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Busanda, Wilaya ya Geita, Dkt. Jafari Rajabu Seif, leo Agosti 25, 2025 amechukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Dkt. Jafari ndiye mgombea aliyeteuliwa rasmi na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa 2025
Baada ya kuchukua fomu, amewashukuru viongozi na wanachama wa CCM kwa imani waliyoonyesha kwake na kuwaomba wananchi wa Jimbo la Busanda kumpokea kwa ushirikiano ili aweze kuwatumikia ipasavyo
“Nitakwenda kuisimamia vyema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha ndani ya Jimbo la Busanda inatekelezwa ili wananchi waendelee kufurahia maendeleo,” alisema Dkt. Jafari.
Ameongeza kuwa ataimarisha mahusiano kati ya mwakilishi na wananchi na kuhakikisha Jimbo la Busanda linapendeza kwa miradi na huduma zitakazotekelezwa kupitia Ilani ya CCM
0 Maoni