Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Mhoja Mapande akimtua ndoo mama kichwani ikiwa ni uzinduzi wa bomba la maji kata ya ludete

Serikali kupitia uwekezaji wa Shilingi Bilioni 6 imefanikisha kuanza kazi kwa Mradi wa Maji wa Katoro-Buselesele, ambao sasa unahudumia zaidi ya wakazi 12000 na kupunguza changamoto ya maji katika maeneo ya Katoro, Ludete, na Nyamigota.

Akizungumza wakati wa ukaguzi uliofanywa na Kamati ya Siasa ya Halmshauri kuu ya CCM Wilaya ya Geita  katika eneo la Bugaya mbelele A kata ya Ludete, Mkurugenzi Mtendaji wa GEUWASA, Frank Changawa, amesema  mradi huo umekamilika kwa asilimia 98 na kwa sasa unazalisha lita milioni 2.5 za maji kwa siku, huku ukiwahudumia wateja 500 wa taasisi 10.


Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Geita  Frank Changawa akifafanua jambo

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande, aliwataka wananchi waendelee kuamini serikali ya chama hicho kwa juhudi zake za kuleta maendeleo endelevu.



Mradi huu umeonekana kuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo, ukiboresha maisha na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.