Eneo la Mbuga ya Gombe iliyoungua

MBUGA ya Gombe nyumbani asilia kwa sokwemtu imeteketea kwa moto kwa zaidi ya asilimia 60 huku wanyama mbalimbali wakihofiwa kuathiriwa na moto huo.


Akizungumza na The Profile Blog mwananchi ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema Moto umevuka toka nje ya hifadhi na kuingia hifadhini na sasa umeunguza maeneo mengi ndani ya hifadhi nafikiri 60% ya hifadhi imeungua na nikiangazi na chakula kingi cha wanyama kimeungua


"Sokwe wamenusurika ila watateseka kwa mda maana %70 ya chakula chao wanachokitegemea kwa sasa kiangazi kimeungua,kwa wanyama wakubwa kama nyani wenyewe wanakimbia ila wadogo wadogo wanaungua na kufa" alisema mwananchi ambaye hakutaka kutambulika

"Zaidi ya siku ya 6  timu ya wanakijiji na baadhi ya watu kutoka mjini na taasisi mbalimbali tunaukabili"alisema.

Juhudi za kumtafuta Mkuu wa hifadhi ya Gombe kwa njia ya simu hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana.