NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI DOTO BITEKO AKIWA NA MKUU WA MKOA WA GEITA MARTINE SHIGELLA PAMOJA NA DR BARAKA KULWA WAKATI WA UZINDUZI WA JENGO LA UPASUAJI KATIKA HOSPITAL YA CHARLES KULWA MEMORIAL  

NA ROSE MWEKO, BUKOMBE.

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko ametoa pongezi kwa hospitali binafsi kwa kuendelea kutoa huduma za afya kwa wananchi na kuisaidia serikali katika kuhudumia wananchi haswa katika huduma za kibingwa kwa gharama nafuu.

Dkt Biteko ameyesema hayo wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji katika hospitali ya kumbukumbu ya Charles Kulwa iliyopo katika mji wa Runzewe Wilayani Bukombe Mkoani Geita huku akiupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kuboresha huduma mbalimbali.

VIONGOZI MBALIMBALI WAKIKATA UTEPE KUZINDUA JENGO LA UPASUAJI KATOKA HOSPITAL YA CHARLES KULWA MEMORIAL 


Alisema hospitali binafsi zimesaidia kuwafikia wananchi kwa karibu pale ambapo hospitali za Serikali zinakua mbali aidha kutokana na juhudi na kujituma kwa wamiliki wa hosptali hizo kumekuwepo na huduma za kisasa huku wananchi wakipata unafuu wa kupata huduma hizo na hiyo ndio kazi ambayo Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama Samia Suluhu Hassani inakusudia kufanya kuhakikisha inaboresha afya za wananchi kwa kuweka mazingira rafiki kwa watoa huduma mbalimbali kwa jamii.

“kwa dhati ya moyo wangu nipongeze hospitali hii ya Charles Kulwa chini ya Mkurugenzi wake Dkt Baraka Kulwa kwani wamekuwa wakitoa huduma za kisasa na kwa bei inayoweza kufikiwa na wananchi wote hii ndio ile tunayosema Serikali imeboresha mazingira ya utendaji kazi kwa wote kwa maslahi ya wananchi kwani ukiwa Hapa Charels Kulwa unapata huduma nyingi ambazo unaweza kuzipata katika hospitali kubwa hivyo wananchi wa Runzewe na maeneo ya jirani watapata huduma hapa kwa ukaribu na haraka” alisema Biteko.


NAIBU WAZIRI MKUU DKT DOTO BITEKO NA VIONGOZI MBALIMBALI WAKIKATA UTEPE KUZINDUA JENGO LA UPASUAJI KATIKA HOSPITAL YA CHARLES KULWA MEMORIAL 

Dkt Biteko aliwataka watoa huduma wa afya wengine kuiga mfano wa Hospitali ya Charles Kulwa kwani kwa mda mrefu kumekuwepo na utendaji kazi wa hali ya juu bila malalamiko na migongano nah ii yote ni kutokana na kuwepo na uongozi ulio thabiti uliolenga kuwahumia wananchi ambapo kwa upande wake aliahidi kuchangia vitanda vya wagonjwa ishirini huku baadhi ya wadau wakichangia vifaa mbalimbali ambapo nye Kulwa Biteko aliahidi kuchangia mashuka miambili kwatika hospitali hiyo.

Martine Shigella ni Mkuu wa Mkoa wa Geita alisema Serikali itaendelea kuwaunga mkono watoa huduma za afya kwani huisaidia Serikali katika kuwahudumia wananchi na kupunguza mzigo wa ajira kwa Serikali hivyo Mkoa wa Geita utaendelea kutengeneza mazingira rafiki ili huduma ziweze kuwafikia wananchi kwa ukaribu na haraka zaidi.

“nchi yetu inataka ipate wazalendo wengi kama ndugu yetu Dkt Baraka kwani wengi wao wakipata fedha hukimbia nyumbani kwao na kuwekeza mbali lakini tuhahitaji kuwapata vijana kama hawa kwani utoaji wa huduma za hapa ni wa kisasa hivyo kuwezesha kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hosptali ya Kanda aidha kwakuwa uongozi wa hapa umeboresha maslahi ya wafanyakazi hivyo mzigo wa vijana wanaotafuta ajira unapungua niendelee kuwataka wananchi kuwekeza katika sekta mbalimbali Mkoani Geita na uongozi wa Mkoa utawapa ushirikiano” alisema Shigella.

 Awali akisoma taarifa ya hospitali Dkt Mariana Bachillulah alisema kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi  hospital imekua ikifanya kampeni na ushauri wa namna ya kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza hasa kwa watu wenye zaidi ya umri wa miaka hamsini ikiwemo magonjwa ya shinikizo la damu,kisukari na saratani ambapo hospitali ilifanikiwa kuwafanyia vipimo vya awali bure zaidi ya wagonjwa 605 ambapo kati yao wagonjwa 146 wamekutwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

“aidha katika kampeni hiyo tuliweza kuwapata wagonjwa wa kisukari na tezi dume aidha kati ya wanaume 258 waliopimwa wanaume 50 walikutwa na tezi dume ambapo walipatiwa tiba za awali na baadae kufanyiwa upasuaji” alisema Dkt Bachinulwa.

 “ aidha tumeongeza upasuaji mkubwa na mdogo kwa asilimia40 ukilinganisha na mwaka 2022 aidha tunaendelea kuboresha huduma zetu hasa katika kliniki za madakrari bingwa wa magonjwa ya moyo, upasuaji wa masikio,pua na koo huku tukitoa kipaumbele katika magonjwa ya akinamama aidha tumeendelea kuboresha huduma za macho,ngozi na mifupa huku tukiboresha upasuaji wa kibingwa wa magonjwa ya ndani”, alisema Dkt Bachillulah

MWISHO.