
MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUWA WALINZI WA AMANI.
N.A. ROSE MWEKO, GEITA.
KATIBU wa NEC Itikadi, uenezi na mafunzo Paul Makonda amewataka wananchi wa mji wa katoro/Buseresere kuwa walinzi wa amani kwa kuhakikisha wanawabaini na kuwafichua waharifu na watu wanaofanya ukatili wa binadamu katika mji wa katoro na maeneo yote ya kanda ya ziwa ili kuifanya kanda hii kuwa sehem salama ya kuishi.
Makonda alisema mji wa katoro na Buseresere ni mji wa kibiashara unapaswa kuwa na amani na utulivu ili kuwafanya wananchi kufanya kazi za kujitafutia riziki wafanye kwa amani na utulivu ambapo kwa kufanya hivyo Serikali itajiongezea kipato kwa kukusanya kodi.
" ndugu zangu niwaombe kila mtu awe mlinzi wa mwenzie kwa kusimamia ulinzi ikiwemo ni ulinzi dhidi ya waharifu pia ulinzi ulinzi dhidi ya watu wenye kutenda uharifu kwa watoto, wanawake na jamii kwa ujumla kwani vitendo hivi vinadumaza maendeleo ya Taifa" alisema Makonda.
Alipotaka kujua utekelezaji wa mradi wa maji Katoro /buseresere Makonda alimpigia simu Waziri wa Maji Juma Aweso ambapo alisema mradi huo maji umegharimu zaidi ya billion 6 .5 ambapo mpaka sasa ujenzi umeshakamilika kwa aslimia 92 na inatarajiwa kukamilika asilimia 100 ndani ya wiki tatu kutoka sasa .
Aweso alisema kuna mradi mkubwa wa maji utakaonufaisha miji zaidi 28 ikiwemo mikoa ya Kanda ya ziwa na inatarajiwa kuwa mpaka kufikia 2025 mradi huo utakua umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95 ya upatikanaji wa maji safi na salama.
" Geita ina vijiji 486 ambapo mpaka zaidi ya 333 vimeshapatiwa maji na tayari zaodi ya billioni 24 zimeshatolewa ili kutatua changamoto ya maji ambapo tayari Serikali imeshanumua Mitambo 25 ikiwa kila Mkoa ulipatiwa mtambo 1 utakaowawezesha kuchimba kisima katika maeneo ambayo hayatafikiwa na maji mkubwa" alisema Aweso.
" Tanzania ina Vijiji 12318 ambapo tayari vijiji 9675 vimeshapatiwa maji na vijiji 1500 miradi inatekelezwa " alisema Aweso
Katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Barabara
Makonda alimtaka meneja wa TARURA Wilaya ya Geita mhandisi Bahati Subeya kutoa ufafanuzi wa ujenzi wa barabara za mitaani kwa kiwango cha lami
Katika mji wa katoro/ Buseresere Tarura ina kilomita 153 ambapo mpaka sasa Tayari kilomita 2 za lami katoka mji wa Katoro zimeshajengwa kwa gharama ya million 647.
Makonda alisema Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Geita kuongeza bajeti yake TARURA ili kuwezesha kukidhi mahitaji ya utekelezaji wa miradi.
MWISHO
0 Maoni