KATIBU WA NEC ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO PAUL MAKONDA APOKELEWA GEITA.
NA ROSE MWEKO, GEITA
KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amesema Serikali ya Chama Cha mapinduzi chini ya mama Samia Suluhu Hassani inafanya kazj bila ubaguzi wala kuwa makundi hivyo kuwataka watu wanaoeneza propaganda zao waache.
Makonda amesema hayo katika kijiji cha Mganza Wilayani Chato Mkoani Geita wakati wa mapokezo yake akitokea Mkoani Kagera ambapo ikiwa ni ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa iliyoanza tarehe 9 November mwaka huu.
Alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya watu kutengeneza nadharia ya makundi ndani ya chama jambo ambalo mama Samia Suluhu Hassani yeye hana makundi kwani kama angekua na makundi hayo asiweza kumchagua yeye na wengineo.
" Kuna watu wanaeneza propaganda kwa habari ya makundi niwaambie Rais Samia Suluhu Hassani hana makundi ingekua ana makundi asingenichagua mimi katika nafasi hii wala asingeweza kuwachagua wakina Doto Biteko kuwa viongozi mama anataka wachapakazi na sio vinginevyo" alisema Makonda.
" na ninaahidi kuwa sitamuangusha kama alivyoniamini na kuniteua nitafanya kazi kwelikweli na niwaombe ndugu zangu wa kanda ya ziwa tusimuangushe mama yetu Kipenzi chetu tufanye kazi kwabidii lakini pia ifikapo kipindi cha uchaguzi tujitoe kumpigia kura kwa kishindo" alisema Makonda.
0 Maoni