MKUU WA WILAYA YA GEITA CORNRL MAGHEMBE


NA ROSE MWEKO, GEITA.

MKUU wa Wilaya ya Geita Cornel Maghembe amesema Serikali haiwezi kuruhusu watoto kuwepo maeneo ya machimbo ya madini kwani katika maeneo hayo kuna muingiliano wa watu wengi hivyo kuhatarisha makuzi ya watoto kiafya na kimaadili.

Maghembe aliyasema hayo katika eneo la machimbo la nyamatagata lililopo katika kijiji cha Manga kata ya Mgusu, alisema eneo hilo ni hatarishi kwa usalama wa watoto kwani kumekuwepo na mashimo mengi kutokana na shughuli zinazofanyika, aidha kwa kuzingatia maadili na kanuni zinazomlinda mtoto haziruhusu watoto kuwepo katika maeneo hayo kwa ustawi wa maisha yao.

“niseme wazi Serikali haiwezi ikaruhusu watoto kuwepo eneo hili kwani ni eneo hatarishi kwa mazingira yalivyo yapo mashimo, vumbi na kelele za mitambo ni hatari kwa watoto lakini pia ni eneo ambalo halifai katika malezi ya watoto kwani kuna muingiliano wa watu tofauti na wenye hulka zisizofanana hapa panapaswa kuwepo na uchimbaji pekee hivyo kiafya sio salama kwa watoto, niwaombe wanawake ambao mtakua mmebeba ujauzito ikifikia muda wa kujifungua nendeni mkajifungue mkimaliza ulezi mtarudi hatujawafukuza lakini haifai eneo hili kuwa na watoto kwani bado tunawahitaji kwa ustawi wa Taifa la baadae” alisema Maghembe.



Maghembe aliwataka wachimbaji kuendelea kulipia ushuru na michango mingine ya halmashauri ili kuharakisha maendeleo katika maeneo yao, alisema mtu yeyote anapotoa fedha kwa ajili ya ushuru wa Serikali ni lazima adai risiti kwani fedha ya serikali haitolewi kiholela.

“ kuna watu wamenilalamikia kuwa hapa kuna ushuru wa halmshauri unaotolewa kwa namna mbili shilingi elfu mbili unapewa risiti na shilingi elfu moja haupewi risiti halafu kuna mgambo wanakwenda mbele wanawakamata wale wasio na risiti na kuwatoza elfu moja nyingine hapo mnaonaje kwanza niseme unapotoa fedha ya serikali bila kupewa risiti huo ni wizi kwa hiyo unayetoa na kupokea wote ni wezi na kazi ya askari Mgambo ni kukamata nyie mnaotaka bei za mkato na watawakamata ili muone kero ya kuiibia Serikali”

“hivyo mnaiibia Serikali kwa kupitisha mizigo isivyo halali ninaaagiza Mkurugenzi fuatilia hili ukibaini kuna watu wanafanya hivyo fukuza mnaona miradi mingi inajengwa na Serikali kwani fedha hizo zinatoka wapi?  ndio hizo zinazotokana na ushuru mnaotoa wenyewe kwahiyo usipodai risiti unakua umeshiriki kuiibia Serikali na tukikubaini tutakukamata” alisema Maghembe.

Aidha Maghembe aliwataka wawekezaji wa migodi kutenda haki kwa wachimbaji wao katika kuhakikisha wanatimiza ahadi kwani kumekuwepo malalamiko mengi kutoka kwa wachimbaji wakilalamikiwa kutolipwa sawa na makubaliano ambapo katika mifuko kumi yam awe yenye dhahabu wachimbaji wanapaswa kupewa mfuko mmoja kama malipo lakini ajabu ni kupewa pungufu ya makubaliano.



“niwatake wawekezaji hakikisheni mnatenda haki na kutimiza makubaliano mliojiwekea haiwezekani watu wanachimba kwa shida halafu ikifika muda wa mgao nao usiwape kama yalivyo makubaliano ninaagiza kaeni n wachimbaji wenu mkubaliane ili kila mtu apate stahiki yake” alisema Maghembe.

 Awali baadhi wananchi akiwemo Shija Bugomola walimuomba Mkuu wa Wilaya Maghembe kuwasaidia kupunguza mrundikano wa tozo za mirabaha katika migodi midogo kwani hukatwa kodi wanapokusanya mawe pia huwatoza wakati wa uchenjuaji na baadae huwatoza tena wakati wa uuzaji kwa dhahabu ile ile jambo ambalo linawaumiza wawekezaji.

“mheshimiwa Mkuu wa Wilaya sisi wachimbaji wadogo tumekuwa tukikatwa tozo za mirabaha nyingi kuliko ilivyo kawaida wanakata asilimia zao kuanzia mawe kwanini wasifanye kama inavyofanyika kwa GGM tozo ya serikali ikatozwa pale wakati uzalishaji umekamilika ila kwetu sisi ni tofauti unakatw mno mpaka unaikosa faida halisi tunaomba mtusaidie kwa hili” alisema Bugomola.

MWISHO