NA ROSE
MWEKO, KAHAMA.
NAIBU WAZIRI STEPHEN BYABATO AKIKATA UTEPE KUZINDUA UWASHWAJI WA UMEME KWA MARA YA KWANZA KATIKA KIJIJI CHA BUTONDOLO JIMBO LA MSALALA WILAYANI KAHAMA MKOANI SHINYANGA.
ZAIDI ya Trillioni sita 6.5 zimetengwa kwa ajili ya kupeleka umeme katika vitongoji vyote Tanzania nzima katika mwaka wa fedha wa 2023-2024 lengo likiwa kuiondoa nchi gizani na kuwafanya wananchi kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.Hayo ameyasema
Naibu Waziri wa Nishati Steven Byabato
alipokuwa katika ziara ya kukagua na kuwasha umeme katika jimbo la Masalala
Wilayani Kahama, ambapo kwa jimbo la Msalala pekee zaidi ya billion 18
zimetengwa illi kukamilisha miradi ya umeme jimboni hapo.
“ Mh Rais
Dkt Samia Suluhu Hassani amesema hivi anataka kabla ya kufika 2025 kila kijiji
nchini kiwe kimewashwa umeme na ndio maana amepeleka fedha nyingi katika Sekta
hiyo hii itasaidia kurahisisha kazi mbalimbali na ikizingatiiwa kuwa jimbo hili
ni wakulima wazuri wa mpunga tunataka
wakulima wa vijiji vya Butondolo, Jana na vinginevyo waanze kuchakata mpunga
hukuhuku na kupeleka Kahama mchele hiyo itasaidia kuongeza thamani ya bidhaa
zetu” alisema Byabato.
Byabato
alisema awali Serikali ilikua imetenga shilingi
trillion moja na billion miambili na arobaini lakini Rais Samia
aliposikia kilio cha wananchi kulingana na uchache wa miundombinu iliyopelekwa
vijijini aliamua kuongeza kilomita mbili kwa kwa kila kijiji na hivyo kupelekea
ongezeko la fedha la zaidi ya billion
miatatu na hivyo fedha iliyotolewa ni shilingi trillion moja na zaidi ya billion miatano.
BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA JANA JIMBO LA MSALALA WAKIMSIKILIZA NAIBU WAZIRI NISHATI STEPHEN BYABATO(hayupo pichani) WAKATI WA UZINDUZI WA UWASHWAJI WA UMEME KATIKA KATA TATU
“sasa wenzetu wa REA inawaagiza kufikia
december muwe mmekamilisha miundombinu
yote maana wananchi hawajali nani kaleta umeme katika maeneo yao wanachikitka
ni kuona umeme na sio vinginevyo na serikali kama waumishii wao tuko tayari
kutekeleza hilo hivyo watendaji na wakandarasi ninawaagiza fanyeni kazi kwa
haraka lakini kwa kiwango kinachotakiwa” alisema Byabato.
Iddi kasimu
mbunge wa jimbo la Msalala alisema wananchi wa jimbo la Msalala walifikia hatua
wakaona kuwa wametelekezwa , hii iliwasababishia wao kukata tamaa jambo ambalo
hawakumuamini mtu yeyote aliyefika jimboni hapo kuomba ridhaa ya kuwa
mwakilishi wao hivyo amemuomba Naibu Waziri kuhakikisha anasimamia ahadi ya
umeme kuwaka kil kijiji inatimia.
NAIBU WAZIRI STEPHEN BYABATO AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MKUTANO JIMBO LA MSALALA.
“kama
mnakumbuka tulifika Msalala kuwaomba kura na tuliahidi kuwaletea maendeleo
nanyi mkatuamini mkatupa kura sasa ni wajibu wetu kutekeleza yale tuliyoyaahidi
ikiwemo kuwaletea umeme, afya , elimu na maendeleo mbalimbali na ndio maana leo
tuko na Naibu Waziri wa Nishati amekuja kuzindua uwashaji wa umeme katika kata
zetu tatu na niwahakikishie tu kuwa huu ni mwanzo mengi mazuri mtayaona”
alisema Iddi Kasimu Mbunge wa jimbo la Msalala.
ALHAJI IDDI KASIMU MBUNGE WA JIMBO LA MSALALA AKIFAFANUA JAMBO KATIKA MKUTANO WA HADHARA.
MWISHO
0 Maoni