MKUU WA MKOA WA KAGERA HAJJAT FATMA MWASA

Mkuu wa mkoa wa kagera Ajat Fatma Mwassa amemwagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashari ya Wilaya Biharamulo Denis Mkandala ahanzishe mchakato mpya wa ujenzi wa shule ya msingi katika kata ya Nemba kutokana na changamoto zinazoikabili shule ya msingi Nemba kwa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 4,900 huku ikiwa na vyumba vya madarasa 33 tu.

 

Mwassa  ametoa kauli hiyo katika ziara yake wakati akihutubia wananchi wa kata ya nemba wilayani biharamulo baada ya kupata taarifa ya kata hiyo na changamoto zinazowakabili wanafunzi ikiwemo hatari ya magonjwa ya mlipuko, utoro shuleni na ufahulu hafifu kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi

 


Mkuu wa Wilaya Biharamulo ACP Adivera Bulimba amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo kupitia mradi wa boost wilaya hiyo imepokea fedha kutoka serikali kuu zaidi ya milioni 106 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne na matundu matatu ya vyoo katika shule hiyo

 


Katika kuendeleza elimu mkoani humo mkuu wa mkoa wa Kagera Ajat Fatuma ameanza kwa kuchangia matofari 2000 pamoja na mkuu wa wilaya hiyo matofari 1000 yatakayosaidia ujenzi wa vyumba vitatu vipya vya madarasa

 

MWISHO.