JAMII imeshauriwa kuachana na tabia ya kujenga makazi yao karibu na  maeneo ya hifadhi za mbuga za wanyamapori ili kujiepusha na hatari zitakazo tokana na wanyama wakali na waharibifu kama Tembo,Nyati,Mambana Kiboko.

Kauli hiyo imetolewa na Mhifadhi Mkuu anaesimamia Dawati la Ujirani Mwema kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) PC Twaha Twaibu wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari Kwa nyakato tofauti Jijini Dar es salaam juu athari za kufanya shughuli za kibinadamu karibu na hifadhi za wanyamapori

Mhifadhi Twaha Twaibu ameitaka jamii kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa wanyamapori hao kwaajili ya kuepukana na madhara  yatakayotokana na Wanyamapori hao

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa haraka pindi Wanyamapori hao watakapoingia katika makazi  na kucha tabia ya kupiga nao picha kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao

Katika hatua nyingine Mkuu huyo anaesimamia dawati la Ujirani mwema kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Twaha Twaibu ametumia fursa hiyo Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi-TAWA kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dakta Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara katika masuala ya uhifadhi,Kwani Kwa kipindi alipokuwa Makamu wa Rais ndiye aliyezindua Jeshi la Uhifadhi.