Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo tarehe 15 Mei, 2023 amewasili wilayani Bukombe mkoa wa Geita kwa ziara ya siku moja na kuzindua majengo mbalimbali ya Chama Cha Mapinduzi ikiwemo ukumbi wa mikutano, nyumba ya kupumzika wageni (Rest House) na mgahawa (Restaurant).
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Issa Ussi Gavu. Ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Geita
0 Maoni