Mkurugenzi Halmashauri ya Muleba - ELIAS KAYANDABILA akikabidhi kitabu cha siku 730 za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya serilika kwa Mtendaji wa Kata.
Mauaji,mabishano
na mapigano imetajwa kuwa sababu kubwa ya kurudisha nyuma uchumi na maendeleo
wilaya Muleba huku siku 730 za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zikitumika kama
njia ya kutegua kitendawilihicho ambacho kimekuwa gumzo kwa wakazi ndani ya
wilaya hiyo.
BAADHI YA WAFANYAKAZI NA WANANCHI WAWILAYA YA MULEBA WAKIFUATILIA HAFLA YA SIKU 730
Akizungumza
wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka miwili ya Rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani, Katibu tawala wa
Wilaya ya Muleba Greyson Mwengu amesema serikali haipo tayari kuona vitendo
hivyo vinaendelea katika wilaya ya muleba na kusema kuwa watakuwa wakali zaidi.
Katibu tawala wilaya Mleba - GREYSON MWENGU
0 Maoni