NA ROSE MWEKO, GEITA.
SEKRETALIET YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA GEITA IMEFANYA ZIARA YA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA KATIKA KATA MBILI ZA KASAMWA NA NYANKUMBU LENGO IKIWA KUIMARISHA CHAMA KUANZIA NGAZI YA SHINA.
KATIBU WA CCM WILAYA YA GEITA TIMOTHY SANGA AMESEMA UHAI WA CHAMA HUANZIA KWA KWENYE SHINA HIVYO KINATHAMINI MCHANGO MKUBWA WA BALOZI NDIO MAANA KAMATI TENDAJI INATEMBEA KATIKA MASHINA ILI KUIBUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI NA KUZITAFUTIA UTATUZI.
KATIKA ZIARA HIYO SANGA ALIGAWA BENDERA KWA MABALOZI ILI WAWEZE KUZISIMIKA AMBAPO SAMBAMBA NA HILO ALIWATAKA MABALOZI KUITISHA VIKAO MARA KWA MARA KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO ZA WANACHAMA HUKU AKIAHIDI KUSHIRIKIANA NAO PALE ATAKAPOSHIRIKISHWA.
BAADHI YA MABALOZI WAMELALAMIKIA CHANGAMOTO YA KUKOSEKANA UMEME LICHA YA NGUZO KUPITA KATIKA KIJIJI HICHO AIDHA WAMEIOMBA SERIKALI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA MAJI KWANI UMEKUA KERO KUBWA HASA WAKATI WA KIANGAZI AMBAPO WANAWAKE HUTOKA AFAJIRI KWENDA KUTAFUTA MAJI NA KURUDI KWA KUCHELEWA.
Mwisho.
0 Maoni