NA ROSE MWEKO , GEITA.
KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita Timothy Sanga anakaribisha taasisi, mashirika,kampuni au watu binafsi kuingia ubia na baraza la wadhamini la chama cha mapinduzi kuwekeza katika ujenzi wa majengo ya biashara katika eneo la sabasaba Geita mjini barabara ya Nyerere kitalu namba 90 block c.
mbia atashiriki kujenga frem za maduka 160 ambapo kutakuwepo maduka, ofisi migahawa, supermarket na uwekezaji mbalimbali wa kibiashara, hivyo chama cha mapinduzi kimedhamiria kuwekeza katika mradi wa ujenzi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuboresha biashara katika mji wa Geita.
Sanga alisema kuwa shabaha ya chama cha mapinduzi nikuhakikisha kuwa kinatekeleza na kinafanikisha mambo ya kimaendeleo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama kwa ahadi walizo zitoa kwa wananchi.
Alisema shabaha ya kila Mkoa na jumuia zake ni kuhakikisha zinajitegemea kipato na kiuchumi hivyo inapaswa kuwa na uwekezaji unaotoa lejesho kubwa na wenye tija,hii itasaidia chama Wilaya kuweza kujitegemea katika kuendesha shughuli zake kwa kuona hivyo Wilaya ya Geita inatarajia kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa maduka ambao utajumuisha shughuli mbalimbali,mradi huu utachochea maendeleo kwa Wilaya ya Geita pia utapendezesha madhari ya mji.
“mkakati nikuhakikisha kuwa maeneo yote ya ardhi ya chama na mali yanasajiliwa na kumilikishwa kisheria ili kuweza kuyaboresha kisasa jambo hili litaimarisha uchumi wa chama na kukifanya chama kistawi kupitia miradi na vitenga uchumi vyake vitakavyoanzishwa kwa kutumia raslimali za chama zilizopo,
“Chama cha mapinduzi ni miongoni mwa taasisi nchini zinazomiliki maeneo mengi na mkubwa ya ardhi na kumiliki idadi kubwa ya ya majengo nchini eneo hilolitachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya ndani ya chama frusa hiyo ya aridhi na majengo itabeba tafsiri pana ya uwekezaji katika Mkoa wa Geita”.
Sanga alisema masharti ya mwombaji atapaswa kuwa na uwezo wa kifedha wa kujenga majengo kulingana na mkataba, aidha mwombaji anapaswa kuwa raia wa tanzania ambaye hana rekodi ya uhalifu
0 Maoni