MKUU WA MKOA WA GEITA MARTINE SHIGELA.
WANANCHI FANYENI KAZI MCHAKATO WA KUUGAWA MKOA WA GEITA NI MGUMU.
NA ROSE MWEKO.
MKUU wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wananchi kuacha kufikiria kuugawa Mkoa na badala yake wajikite katika kutafuta maendeleo kwani mchakato wa kuugawa Mkoa wa Geita katika Wilaya za Chato umekua mgumu baada ya Mkoa wa Kagera kugoma kutoa Wilaya zake tatu za Muleba Ngara na Biharamulo huku Mkoa wa Kigoma ukitoa sharti la kuwa iwapo Chato inataka kuanzishwa ili Kigoma itoe eneo lake la Wilaya ya Kakonko basi makaomakuu ya Mkoa yawe Nyakanazi.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Geita Shigela alisema Mkoa wa Geita hauna mamlaka ya kulazimisha mikoa mingine ikubali kugawa maeneo yake zaidi ya kutoa mapendekezo Wizarani ambapo napo huzingatia maoni kutoka katika Mikoa mingine jambo ambalo kwa sasa limekua gumu baada ya Mkoa wa Kagera kugoma kutoa maeneo yake huku Kigoma ikitoa Wilaya ya Kankoko kwa masharti.
WAJUMBE WA KIKAO CHA USHAURI CHA MKOA“katika vikao mbalimbali huko nyuma vya kamati ya ushauri Mkoani kwetu tuliazimia kuwa mapendekezo y uanzishwaji wa Mkoa mpya yawasilishwe ofisi ya Rais TAMISEMI ili hatua za uanzishwaji wa Mkoa huo zianze ambapo kwa mujibu wa taarifa TAMISEMI walisema kwa sasa haiwezekani Mkoa wa Chato ukaanzishwa hivyo mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Geita siwezi kuwapa matumaini hewa ambayo hayana mwanga mbele nitakua sio kiongozi” alisema Shigela.
“hatuna mamlaka ya kwenda kuongea na watu wa Biharamulo wala Kakonko wenye mamlaka ndio wenye kuweza kuwaandikia mikoa yao kuridhia sasa TAMISEMI walioandikia Mkoa hiyo wao wakajibu hatuko tayari kuachia maeneo yetu na mimi niseme moni hayo yalitolewa na Wilaya ya Chato na sio maoni yetu maombi yetu tulishajibiwa kuwa wenye maeneo mengine hawataki, kama Mkoa wetu ungekua ni mkubwa tuseme tuugawe hap sawa sasa kama tunaona Mkoa wetu ni mdogo na haugawiki kwanini tuhangaike kuugawa tujenge uchumi wetu tutatue changamoto zetu” alisema shigela.
WAZIRI WA MADINI DKT DOTO BITEKO NA MKUU WA MKOA WA GEITA MARTINE SHIGELA WAKITETA JAMBO WAKATI WA KIKAO CHA RCC GEITAMkoa wa Geita uliwasilisha BaruaTAMISEMI yenye kumb CAB.131/319/01/39 ya mei 31 2021 ikiomba Wizara kutekeleza agizo hilo ambapo Ofisi ya Rais TAMISEMI ilitoa mrejesho kwa barua yenye kumb namba CBD.132/503/01B/26 ya oct28 2022 ikielezea kuwa kamati ya ushauri ya Mkoa wa Kagera haijaridhia kutoa maeneo yake ya Wilaya tatu kupelekwa katika Mkoa Mpya wa Chato huku Mkoa wa Mwanza ukigoma kutoa eneo la Wilaya yake ya Sengerema kuwa Mkoa wa Geita isipokuwa Wilaya moja ya Buchosa.
“Mkoa wa Tanga una halmashauri 11 una majimbo ya uchaguzi 12 tarafa 37 na kata 245 mara mbili ya mkoa wa Geita lakini sijasikia habari ya kuugawa Mkoa hata Mkoa wa Morogoro pia ni mkubwauna halmashauri 9 kata 224 na inaukubwa wa eneo elfu 73 mara tatu na zaidi ya Geita ila huo mjadala haukuwepo huku Geita ikiwa na ukubwa wa eneo elfu 21 ndugu zangu tusiwekeane matumaini ambayo hayapo tuwaambie wananchi wet wachape kazi hizi habari za kuugawa Mkoa mchakato wake bado ni changamoto” alisema Shigela.
Awali Mbunge wa Chato Dkt Merdad Kalemani ameomba mapendekezo ya kikao cha RCC Mkoa iridhie kutoa mapendekezo ya kuridhia Mkoa wa Chato ugawanywe ili iwe rahisi kwa mikoa mingine kukubali kutoa maeneo yake kama ambavyo ilitarajiwa ili ngazi za juu za maamuzi ziweze kuruhusu kwa hatua zaidi za utekelezaji.
“ mimi ningeomba kamati yetu ya ushauri ipeleke mapendekezo ya kuwataka wenzetu wa mikoa ya jirani iliridhie kugawanywa kwa mkoa wa Chato ili ibakie ngazi za maamuzi zitoe maelekezo ya utekelezaji kwani ni Mkoa mmoja tu ambao haujaridhia kutoa eneo lake huku Mkoa wa Kigoma ukitoa eneo kwa masharti kimsingi ni kama wamekubali japo kwa sharti lao itakuwa ngumu kwani maandalizi ya miundombinu kwa kiasi kikubwa yamefanyika Wilayani Chato sasa kuipeleka tena Nyakanazi itakua ngumu” alisema Dkt Kalemani.
MWISHO.




0 Maoni