NA ROSE MWEKO, GEITA

 


DARAJA LA KIGONGO-BUSISI LIKIWA KATIKA HATUA MBALIMBALI ZA UJENZI.

(picha na Rose Mweko)

MKUU wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewaambia wananchi wa Geita wajiandae kuchngamkia fursa za kiuchumi kutokana na daraja la Kigongo- Busisi kukamilika ujenzi wake kwani uwepo wa daraja hilo utarahisisha safari za kwenda Mwanza na Mikoa ya jirani.

Shigela aliyasema hayo juzi katika kikao cha 13 cha bodi ya barabara Mkoani Geita alisema daraja hilo likikamilika litaifanya Geita kwa lango uu la biashara na nchi jirani hivyo kuwataka wananchi kuwa katika utayari wa kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta ambapo maandalizi ya ulipaji wa fidia kwa wananchi unaendelea.

“tunawataka mamlaka za usimamizi wa barabara kuendelea kuwajibika na kusimamia sheria ili kuzilinda barabara zetu hii itasaidia kuboresha huduma katika sekta hii aidha elimu ya matumizi sahihi ya barabara iendelee kutolewa kwa wananchi ili kuepuka mkanganyiko wa matumizi sahihi ya barabara” alisema Shigela.



Daraja la Kigongo- Busisi maarufu kama daraja la Magufuli linaendelea kujengwa kwa kasi ya kuridhisha huku mafundi wakionekana kuendelea na ujenzi huo kwa kasi.