BAADHI YA WAOMBOLEZAJI WAKIWA UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA WAKATI WA KUAGA MIILI 19 YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE YA PRECISION AIR MJINI BUKOBA MKOA WA KAGERA
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakati wa kuaga miili ya Watu 19 waliofariki kwenye ajali ya ndege Bukoba jana, amewahakikishia Watanzania kuwa usafiri wa anga nchini upo salama sana na kuwataka waendelee kutumia ndege kusafiri.
“Timu ya Wataalamu tangu jana ipo eneo la ajali na uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea, Watanzania kwa sasa tuwe
watulivu wakati uchunguzi unaendelea, ukikamilika tutaeleza kwa kina chanzo cha ajali hiyo”
BAADHI YA WAOMBOLEZAJI WAKIWA UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA WAKATI WA KUAGA MIILI YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE YA PRECISION AIR MJINI BUKOBA“Uwanja wa Bukoba upo vizuri na salama sana, hivi sasa tuko kwenye hatua za mwisho kuondoa ndege ya Precision Air kwenye uwanja huo kwa sasa ndege ndogondogo zina uwezo wa kutua na kuruka kwenye uwanja huo, hata Mimi jana jioni niliutumia uwanja huo, tulikuwa na ndege yenye abiria 30 na tumetua salama”
“Naamini mpaka ikifika jioni ya leo ndege ya Air Tanzania inaweza kutua na kuruka kwenye uwanja huo, niwahakikishie Watanzania wenzangu, usafiri wa anga nchini upo salama sana, ndio usafiri salama sana duniani, tuendelee kutumia usafiri huu wa anga, iliyotokea jana ni bahati mbaya sana na tunaamini huko tunakokwenda haitotokea tena”
0 Maoni