Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amesema Serikali imepokea maoni ya Wananchi ya namna Serikali inavyotakiwa kuboresha mifumo ya uokoaji, na Serikali imeyachukua maoni hayo na inaenda kuyafanyia kazi.
“Katika tukio lolote zuri na baya ni fursa ya kujifunza, katika janga hili lenye majonzi makubwa, tumepokea maoni ya Wananchi ya namna tunavyohitaji kuboresha mifumo ya uokoaji, na Serikali hii sikivu inayoongozwa na Rais Samia, maoni haya tumeyachukua tunaenda kuyafanyia kazi”
“Jitihada za rasilimali za uokoaji tumeona jinsi Sekta binafsi ilivyoshiriki katika zoezi la uokoaji huu, kupitia Kurugenzi ya maafa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na sisi upande wa Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama tunaenda kujipanga kuhakikisha tunashirikiana na Sekta binafsi”
“ Tutajipanga kuhakikisha tunakuwa na kanzidata ya vifaa vya uokoaji ili maafa yanapotokea tuwe tayari kukabiliana nayo”EBa
0 Maoni