.KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA GEITA LEONIDAS FELIX
*kisa matumizi mabaya ya ofisi
*afutiwa dhamana kwa kukiuka masharti
NA ROSE MWEKO, GEITA.
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita 2014-2016 Magreth Nakainga amefutiwa dhamana yake na hivyo kuwekwa chini ya ulinzi kufuatia kesi inayomkabili ya matumizi mabaya ya ofisi ambapo alihusika kuhujumu mradi wa ujenzi malisho ya mifugo .
Akizungumza na waandish wa habari Kamanda wa Takukuruu Mkoa wa Geita Leonidas Felix alisema wakati wa utumishi wake kama Mkurugenzi wa Mji Nakainga alikiuka utaratibu wa bodi ya wazabuni unaotakiwa kupitisha maombi ya kandarasi zinazoombwa na badala yake yeye na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyoMartine Kwilasa na kukiuka maamuzi yaliyokuwa yamepitishwa na bodi ya wazabunikupitisha mradi huo.
“pamoja na wao kujigeuza kama bodi ya wazabuni na kufanya maamuzi yaliyo kinyume na maamuzi ya bodi ya wazabuni bado hata mradi huo haukujengwa nay eye alidhani kwakua amestaafu basi hakuna kesi yeyote itakayomfuata, nipende kuwaambia tu kuwa jinai haifi mpaka pale mtu atakapofariki hivyo niwaombe wananchi kuwa waadilifu hasa mnapokuwa mmekabidhiwa dhamana ya kuongoza taasisi yoyote” alisema Felix.
Wakati huohuo takukuru imeendelea kupokea malalamiko na kuyafanyia uchunguzi ambapo katika kipindi cha julai hadi septemba Takukuru imepokea malalamiko sitini na moja ambapo taarifa zinazohusiana na makosa ya rushwa ni 36 na zile zisizohusiana na makosa ya rushwa ni 25.
Aidha sekta zinazolalamikiwa ni serikali za mitaa ambapo jumla ya malalamiko 22 yamelalamikiwa huku sekta zingine zikilalamikiwa na makosa 39, aidha taarifa hizo zinaendelea kufanyiwa uchunguzi na zipo katika hatua mbalimbali ambapo taarifa 3 zimefungwa baada ya kukosa ushahidi.
“katika kipindi hiki keshi tatu zimefunguliwa mahakamani na kufanya jumla ya kesi zilizoendeshwa mahakamani kufikia kesi 16 huku kesi mbili zikitolewa hukumu na jamhuri kushinda na hivyo tunawaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa ofisi ya takukuru ilikuhakikisha haki inapatikana bila rushwa” alisema Felix.
Aidha takukuru imejipanga katika kipindi cha kuanzia septemba na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia takukuru inayotembea mradi ambao utawawezesha wananchi wengi kupata elimu juu ya makosa yanayohusianishwa na rushwa na hivyo itakua rahisi kwa wananchi kutoa ushirikiano.
“tutaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hasa ile miradi ya kimkakati hasa katika miradi ya maji, elimu na afya ili kuwawezesha wananchi kupata huduma ya haraka na iliyo bora kama ambavyo imekusudiwa na serikali aidha tunatarajia kuendelea kuwafikia wananchi na wadau mbalimbali kupitia warsha, semina na akongamano mbalimbali ili kufikia makubaliano ya namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika maeneo yao ya utendaji ambayo uchambuzi wa mifumo umebainisha kuwepo na tatizo la viashiria vya kupatikana kwa rushwa”alisema Felix.
MWISHO
0 Maoni