Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko amewapongeza TBA na kuwapa ushauri ili kuongeza ufanisi katika kukamilisha miradi kwa wakati na yenye kiwango na kukabidhi kukabidhi majengo kwa ajili ya kutumiwa na wahusika kutekeleza majukumu ya kutoa huduma.
Dkt Biteko aliyasema hayo alipotembelea banda la TBA katika maonesho ya 5 ya teknolojia ya madini Mkoani Geita wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo ambapo Biteko alikua akimuwakilisha Rais Samia Suluhu Hasan
"Niwapongeze TBA kwa miradi mbalimbali ya ujenzi mnayoifanya hasa katika Mkoa wa Geita lakini niwatake muongeze kasi na ufanisi katika kazi zenu ili kuaminika namkujitanua zaidi mkizingatia kuwa ninyi ni taasisi ya Serikali ",alisema Dkt Biteko
Nao wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamewahahakikishia wananchi kuwa wataendelea kujitanua zaidi kwa kubuni, kutathimini, kutekeleza na kusimamia miradi ya ujenzi kwa ufanisi kwani serikali imeweka mazingira wezeshi kwao TBA kuwajibika kikamirifu.
Ofisa Mawasiliano na Ushirikiano wa TBA, amesema hayo katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya Bombambili Mjini Geita.
Alisema tayari serikali imeshafanyia kazi changamoto zilizokuwepo TBA ikiwemo uhaba wa watumishi, vitendea kazi na viwanda vya kuzalisha raslimali ujenzi hivo wana uhakika miradi yote wanayosimamia inakamilika kwa wakati.
“Pale katika mji wa serikali Mtumba Dodoma tmefanya mradi wa majengo ya serikali na wizara 28, ambapo moja ya jengo hilo ni ofisi za wizara ya madini, ambapo kwa sasa tunafanya usimamizi na mradi huo umefikia asilimia 58 ya mradi.
“Tuna majengo matatu ambayo tumeyajenga katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita, lakini tuna majengo matano ambayo tumeyajenga katika hospitali ya rufaa ya kanda Chato na majengo sita ya ofisi mbalimbali hapa mkoani Geita.
“Vilevile tuna mradi mkubwa wa nyumba za watumishi 3500 pale Nzuguni Dodoma, ambapo hapa tumekuwa tukiwaonyesha wananchi pamoja na atumishi ambao wanafanya kazi na wamekuwa na shauku la kuona mradi huo.” Amesema
Ameongeza “Tuna watalaamu wa kutosha, tuna wataalamu ambao wana ajira za kudumu serikalini, lakini vile vile tulipata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kuajiri wafanyakazi wengine kwenye miradi kwahiyo imetuongezea nguvu ya kutekelza majukumu yetu.”
Alisema TBA chini ya Wizara ya Ujenzi tayari wamekamilisha ununuzi wa mitambo muhimu na ujenzi wa viwanda viwili vya kuzalisha raslimali ujenzi ikiwemo tofari na zege vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma.
MWISHO
0 Maoni