NA ROSE MWEKO,Geita
KATIBU Tawala wa
Mkoa wa Geita Profesa Godius Kahyarara amewahamasisha wananchi na wanachimbaji
wadogo wa Madini kujiunga na mafuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya
kujiwekea akiba ya sasa na ya baadae.
Akizungumza na
wanufaika na wajasiliamali pamoja taasisi za kifedha kupitia siku maalumu ya
Nssf DAY yenye lengo la kutoa elimu kwa wajasiliamali hao na wachimbaji wa
madini katika Maonyesho ya tano ya teknolojia ya Madini mkoani Geita, Kahyarara
amesema ni vizuri makundi ya wachimbaji wadogo pamoja na wananchi kwa ujumla
kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanajiunga katika mifuko hiyo ya hifadhi
ya jamii jambo ambalo litawapa faida ya kuweka akiba kwa maisha ya baadae.
"Nawapongeza
Nssf kwa kuja na utaratibu huu wa kutoa elimu kwa wajasiliamali na hasa yenye
lengo la kuwakumbusha umuhimu wa mifuko ya hifadha ya jamii,hivyo sisi kama
mkoa tumeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha tunawajengea uwezo katika
shughuli zenu mnazozifanya na kubwa nijiunga na mifuko ya hifadhi hususani Nssf
Kwa ajili ya akiba ya uzeeni."amesema Professa Kahyarara
Kwa upande wake
Meneja Uhusiano Elimu kwa Umma (NSSF) Lulu Menegele akizungumzia siku ya Nssf
kupitia maonyesho ya Madini amesema kuwa lengo la siku hiyo nikuendelea
kuongeza uelewa kwa wanachama na wachimbaji wadogo wamadinini kujiunga na mfuko
wa hifadhi ya Taifa ya Jamii Nssf.
MENEJA UHUSIANO ELIMU KWA UMMA NSSF) LULU MENGELE
Amesema kuwa
wametumia fursa ya maonyesho hayo kutoa elimu juu ya mfuko wa jamii na kuelezea
umuhimu wa namna ya kujiunga na mfuko huo nakwamba leo ni kijana na kesho ni
mzee hivyo ukijiwekea akiba ya baadae na ili mwanachama awe hai lazima achangie
"Tumewafikia
wananchi wa mkoa wa Geita ambapo wachimbaji asilimia kubwa sehemu ya wanachama
wa mfuko wa hifadhi ya Jamii na kuhusu huduma zao wanazitoa kwa njia ya
mbalimbali ikiwamo nji ya simu ya kiganjani na hata simu ndogo unaweza kutumia
kujiunga na Nssf."amesema Lulu
Pia ametoa rai
kwa wananchi wa mkoa wa Geita kujiunga na mfuko huyo na huduma hizo zinapatikana
kwenye ofisi zote na mfuko zilizopo nchi nzima huku akiwasihi kuendelea
kuzungukia kwenye banda lao ili kuendelea kupata elimu zaidi ya mfuko wa Nssf.
Kwaupande wake
Meneja wa Nssf mkoa wa Geita Winniel Lusingu Amesema kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Nssf hususani mkoa wa Geita unaendelea kuwahimiza wananchi kutambua umuhimu wa
kujiunga na mfuko huo kwa kuwa unafaida kubwa katika maisha.
Ameongeza kuwa
kupitia maonyesho ya Madini wanaendelea kuandikisha wanachama wapya kwa gharama
ya shilingi 20,000 huku wakizingatia kauli mbiu ya ''huduma bora kipaumbele
chetu''
"Mfuko wa
Hifadhi wa Jamii Nssf Mkoa wa Geita tunaandikisha wanachama lakini kisha
tunapinga rushwa kwa nguvu zote na katika hili nawaomba wanachama wetu kufika
kwenye banda letu lililopo hapa kwenye viwanja vya maonyesho na ofisi zetu
zilizopo hapa Geita ili kupata huduma zetu."amesema lussingu
Kwa upande wake
Meneja wa Sekta isiyo rasmi NSSF Makao Makuu Rehema Chuma amesema kuwa Nssf
Inafikia makundi mbalimbali ya wajasiliamali likiwemo kundi kubwa la wachimbaji
wadogo la madini ya dhahabu kuwapa elimu na kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo
ili waweze kunufaika nakuona shughuli ya uchimbaji ina tija.
Pia Rehema
amewahamiza wajasiliamali hao hususani wanachama kujishughulisha na shughuli
itakayomuwezesha kuchangia mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nssf ili baadae ayaone
manufaa lakini pia akiwa na mchango wake kwenye mfuko anaweza kukopesheka na
taasisi mbalimbali za kifedha.
"Ndugu zangu
wajasiliamali na wanachama wa mfuko huu huduma
nyingine ambayo mnanufaika nayo ni mafao ya walemavu,wajawazito,na wenye
matatizo mbalimbali wananufaika na mafao haya hivyo nawaasa kuchangamkia fursa
hii muhimu na pia kuwekeza Nssf kwa ajili ya Malengo yenu ya baadae kwani
masikini wa leo ni utajiri kesho.."amesema Rehema
Pia katika warsha
hiyo amesisitiza makundi mbalimbali kuendelea kujiunga mfuko huo ili kujijengea
maisha ya sasa na ya baadaye huku baadhi ya mnufaika wa mfuko huo Christopher
Gonya alipata fursa ya kuzungumzia mafanikio yake kupitia mfuko huo nakuhamisha
wengine kujiunga nao.
mwisho.
0 Maoni