NGOMA YA ASILI YA KUCHEZA NA NYOKA ILICHEZWA KATIKA HAFLA YA SIKU YA GEITA
Na Rose Mweko, Geita.
MKUU wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema Geita ipo tayari kuwakaribisha wawekezaji watakaoungana na wenyeji kuhakikisha Geita inakua kiuchumi na kuwaletea maendeleo wanageita.
Shigela aliyesema hayo katika siku ya Geita ambayo.ilikua na lengo la kutambulisha fursa, utamaduni na mila na desturi za wanageita katika maonesho ya teknolojia ya madini Mkoani Geita lengo ikiwa kutangaza na kukaribisha wawekezaji.
Aidha wageni walipata fursa ya kutembelea banda la Mkoa wa Geita ambapo waliona ngoma vyakula na kupata masimulizi yanayohusu Mkoa huo.
0 Maoni