MARTIN SHIGELA MKUU WA MKOA WA GEITA AKIFAFANUA JAMBO JUU YA UJIO WA RAIS SAMIA SULUHU HASSANI
Na Rose Mweko, Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara yake ya kwanza ya kikazi Mkoani Geita kwa siku mbili.
Akitoa taarifa kwa wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema Rais atafanya ziara hiyo siku ya tarehe 15 mpaka 16 October akitokea Mkoani Kagera.
Akiwa Mkoani Geita Rais atazindua hospitali ya kanda ya Chato na kuzungumza na wananchi baada ya kutoka Chato Mh Rais ataelekea mji mdogo wa Katoro ambapo atazungumza na wananchi na kisha kuelekea mjini Geita ambapo atafanya ziara katika kituo kikubwa cha kupoozea umeme cha mpomvu na baadae kuelekea katika kiwanda cha kusafisha na kuongeza thamani ya dhahabu cha GGR ambapo baada ya kutoka hapo atakwenda katika kiwanja cha CCM Kalangalala na kuzungumza na wananchi wa mji wa Geita.
Aidha Shigela amewataka wananchi kujitokeza kwa wingu kumlaki na kumsikiliza Rais Samia atakapokua Mkoani Geita na kila atakaposimama kuzungumza na wananchi.
"Hivyo basi nitumie wasaa huu kuwaalika wananchi wote na makundi yote kujitokeza kwa wingi barabarani kumlaki Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassan na baadae kuungana na viongozi na wananchi katika uwanja wa CCM Kalangalala kumlaki na kumsikiliza atakapokua anazungumza na wananchi", alisema.
"Wapendwa tujitokeza kwa wingi ili kumshukuru Rais Samia kwa kuifungua Geita kwa miradi mbalimbali yenye zaidi ya shilingi billioni 190 inayotekelezwa mkoani Geita na ujenzi wa madarasa 844 na mabweni 2 kwa fedha zinazotokana na fedha za UVIKO 19, mradi wa kusambaza umeme kwenye vijiji 132 na mradi wa maji wa miji 28 kupitia chanzo cha ziwa Victoria" alisema Shigela.
" aidha ujenzi wa mradi wa maji vijijini kwa vijiji 15 na ujenzi wa hospital ya rufaa ya kanda ya Chato aidha ujenzi wa shule 7 ikiwa ni moja kila jimbo kupitia mradi wa Sequip na ujenzi wa majengo matatu ya dharula kwenye hospitali za Wilaya Geita, Katoro, Nyang'hwale na Bukombe huku ujenzi wa jengo la huduma ya dharula ICU katika hospital ya Wilaya ya Geita- Nzera" alisema Shigela.
0 Maoni