MKUU WA MKOA WA KAGERA ALBERT CHALAMILA
NA JOHANSEN BUBERWA,KAGERA
Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Mhe. Albert Chalamila ameagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa
watumishi katika kituo cha Forodha cha Mutukula mpaka wa nchi ya Tanzania na
Uganda kutokana na kubainika kwa baadhi ya Watumishi wasio waadilifu
kushirikiana na raia kughushi nyaraka na kupoteza Serikali mapato.
Akizungumza na
Watumishi wa idara zilizopo katika kituo hicho, Mhe. Chalamila amesema kuwa
mnamo tarehe 29.08. iliundwa kamati ya kuchunguza mwenendo wa usafirishaji wa
mazao kutoka Tanzania kwenda nchi ya Uganda na kubaini kuwepo kwa baadhi ya
watumishi wasio waadilifu, iligundulika baadhi ya watu kuwa na nyaraka feki
ambazo zinatumika kugongwa mihuri kwa kushirikiana na maafisa wa kituo hicho.
JENGO LA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA FORODHA MUTUKULA
“mtuhumiwa mmoja
ambaye si Mtanzania kumiliki mihuri mitatu ya bandia ambapo vyombo vya dola
vinaendelea kumfanyia upekuzi na ambae imebainika kushirikiana na watumishi wa
kituo hiki amesema Chalamila.
Pamoja na hao pia
wapo mawakala wa fedha ambao wahusika uwatumia kutuma fedha kwa watumishi wa
kituo hicho na baadhi ya mawakala wamekiri kufanya vitendo hivyo. Hivyo kumtaka
Kamanda wa Polisi Mkoa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa kuchunguza watumishi wa kituo
hicho kwa kushirikiana na mawakala hao ili kuona katika mitandao na kubaini
mawasiliano yanayofanyika.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ndg. Toba Nguvila amesema kuwa ziara ya kwanza ya Mkuu wa Mkoa alitembelea mpaka wa Mtukula na kuzungumza na watumishi. Katika mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa alitoa maelekezo mengi juu ya uadilifu na nidhamu ya Watumishi katika kusimamia shughuli mbalimbali za kibiashara kati ya nchi na nchi. Na msisitizo mkubwa uliwekwa juu ya kumsaidia Rais Samia kwa vitendo kwa kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kusimamia kanuni na taratibu zinazoendesha kituo cha forodha zinazingatiwa.
0 Maoni