Deo Nsokolo Rais Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) 

 Na Rose Mweko, Dodoma.

 cha wanasheria cha Tanganyika  kwa kushirikiana Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kimeendesha mafunzo kwa wanahabari wa kike kutoka katika club za wanahabari mikoa ya Tanzania bara ili kukuza uelewa juu ya sheria mbalimbali nchini..

 akizungumza na wanahabari hao, Raisi wa Muungano wa klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratias Nsokolo  amewataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha wanaandika Habari mbalimbali zinazohusiana na masuala ya kisheria ili kutoa uelewa mpana wa masuala mbalimbali yanayohusu uelewa Kwa kisheria hapa nchini.

Wakili Mary Mwita mwezeshaji wa mafunzo ya Sheria

alisema kuwa mafunzo hayo yatatoa uelewa mpana wa namna ya  kuandika Habari mbalimbali zinazohusu masuala ya  kisheria hapa nchini  na kuwa sauti kwa wasiokuwa na sauti hasa watu washio pembezoni.

Naye Meneja wa Mradi wa TLS Mackphason Buberwa alisema mafunzo hayo yatawasaidia wanahabari kuendelea kuandika habari kwa kufuata sheria zilizopo bila kumuumiza mtu.


washiriki wakiwa katika mafunzo hayo

"mafunzo haya yatawajengea uwezo mkubwa wanahabari hasa wanawake ambapo watakua msaada mkubwa kwani kumekuwepo na changamoto ya wanahabari kuandika habari zinazopaswa kuandikwa kwa kufuata sheria na data kamili na hii hupunguza umuhimu wa habari hiyo kutokana na kutochimba zaidi"