MH ALBERT CHALAMILA MKUU WA MKOA WA KAGERA

KAGERA

Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert John Chalamila amewataka wazazi na walezi katika mkoa huo kuwa karibu na watoto wao ili kuwasaidia watoto hao kuwa na malezi na makuzi bora yakatakayo leta faida kwa taifa la Tanzania.

Akizungumza katika Hafla ya Mpango Jumuishi,Makuzi,Malezi na Maendeleo ya mtoto iliyo shilikisha Mashirika,taasisi na wadau mbalimbali Mkoani humo amesema kuwa, mapango huo utasaidia kutengeneza mazingira mazuri yaliyosahihi yatakayoweza kuisaidia jamii kuwa na kizazi bora bali wasipo elewa ukweli huo itabaki katika mazingira magumu.

MH TOBA NGUVILA KATIBU TAWALA MKOA WA KAGERA

Katika hatua nyingine amesema kuwa unakuta mtu anamzaa mtoto leo anaenda kumtupa wakati amelea mimba miezi tisa tumboni alafu anamtupa mtoto,  amesema unakuta mzazi mmoja anataka kumkomoa baba yake na akidai kuwa anafanya hivyo hataki mimba yake hataki mtoto, akitoa mfano MUNGU alivyo wa ajabu mtoto anakaa hata siku tano bila kufa porini mpaka jamii inamuokota na kumpeleka kwenye kituo cha watoto yatima.

“Kama unaona hujajiandaa kisaikirojia kuwa mzazi basi usizae na kuzaa kusiwe na dhana katika kichwa chako kwamba umebeba mzigo wa mtu mwingine kwa sababu ya maswala ya kupatikana kwa mtoto yana muhusisha Baba na Mama” alisema Mh Chalamila.

Afisa Maendeo Mkoa Kagera Issa Ndimi amesema kuwa programu hiyo ilipangwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2025/26 na kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari,viongozi wa dini, na kuwasaidia kuifikishia jamii taarifa ikiwa ni lengo la serikali pamoja na kuanzisha kona jumuishi zenye lengo la kuwahusisha watoto na wadau mbalimbali.

 BAADHI YA VIONGOZI MBALIMBALI NA WADAU.

Awali akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Programu jumuishi ya Makuzi,malezi na Maendeleo ya mtoto Katibu tawala Mkoa Kagera Toba Nguvila amesema kuwa mpango huo ulizinduliwa na Mh. Rais kwa kuwakilishwa na Waziri Dkt. Doroth Gwajima ambapo utasaidia katika kuhakikisha watoto wanapata malezi bora hasa katika Mkoa wa Kagera na kama watendaji ndani ya mkoa huo wapo tayari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kuwaomba baadhi yao waanze kwa kuchangia chakula cha mchana shuleni.

MWISHO