Picha ya Kaimu katibu Tawala Mkoa Kagera Nesphory Bwana
akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa kilimo cha kahawa Mkoa
Kagera.
Wakurugenzi wa halmashari zote Mkoa Kagera wametakiwa kununua mashine za kupima Afya ya udongo kuanzia sasa hadi mwezi Desemba mwaka huu ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo cha kahawa.
Akizumgumza na wahitimu 540 wa
mafunzo ya uboreshaji wa kilimo cha kahawa wakiwemo maafisa ugani ngazi ya kata
,kundi la vijana pamoja na wakulima viongozi walio kuwa chini ya Shirika la
Café Africa Kaimu katibu tawala Mkoa Kagera Nesphory Bwana amesema kuwa shirika
la café Africa limenunua vipimo vinenan na kupata leseni ya mwaka mmoja zinazo
saidia kwa sasa amabapo amesema katika halmashari zote moja tu ndo
inakipimo hicho na Serikali ya Tanzania kwa sasa inazalisha wastani wa tani
elfu 50 kwa mwaka inampango wa kuvuka na kuzalisha tani laki tatu za kahawa
safi nchi nzima ifakapo mwaka 2025 na Mkoa huo ukiwa ni miongoni
mwa wazalishaji.
Picha ya wahitimu wakikabidhiwa vyeti
Katika hatua nyingine Bwana Nesphory amewataka Wahitimu wote wa mafunzo waongeze bidii kwenye zao hilo na kuhamsisha wakulima Mkoani Kagera kutokana na mafunzo waliyoyapata kahawa ilimwe kwa wingi ili kifikia mahitaji na mpango mkakati wa serikali.
Mkurugenzi bodi ya Café Africa
Tanzania Dr. Aikande Kwayu amesema kilimo kwa sasa ni uti wa mgongo katika nchi
ya Tanzania ambapo wananchi wengi mategemeo yao yametazama zao hilo na fedha
zinazoingia nchini za kigeni nyingi za kahawa na kutolea mfano miaka 70
hadi 80 iliyopita nchi ilikuwa na tatizo la mafuta ya petrol na dizeli zao hilo
lilikuwa msaada mkubwa, huku meneja wa bodi ya kahawa mkoa Kagera Edmond Zani
amesema kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili idhinisha na kuanzisha
uuzwaji wa zao la kahawa kwa njia ya mnada na kwa sasa wameshauza takribani
tani elf 54 na bei ya juu kufikia 2130.
Picha ya wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa kilimo cha kahawa Mkoa Kagera.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Café Africa Tanzania Dafroza Sanga amsema mwaka 2018 shirika hilo lilingia Mkoani Kagera kwa malengo matano, moja ni kuongeza tija kwa maafisa ugani kuanzia ngazi ya wilaya,kata na wakulima na kufikia walau maafisa ugani wasiopungu 445,mbili ni uzalishaji miche laki sita amabazo walipatia wakulima kwa kipindi cha mika miwili na imesha anza kuleta matokeoa mazuri na mpaka sasa imeonesha huitaji mkubwa kwa wakulima kulingana na malengo,tatu ni kujua Afya ya udongo na wamepewa luzuku na serikali kwa asilimia 50 wameweza kushirikiana na mkoa wamepata vipimo vya udongo vinne vya kisasa,nne na kuwafikia maafisa ugani namna ya kutunza shamaba na kuwafikia wakulima elfu 2250 aslimia 30 wakiwa ni wanawake, tano kuongeza tija na uzalishaji na kupata zao jipya la kahawa.
0 Maoni