NA Rose Mweko, Geita.
MKUU wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka viongozi na watendaji Mkoa wa Geita kuwa na ushirikiano na mshikamano katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana ili kuendana na kasi ya ukuaji wa uchumi.
Shigela ameyasema hayo alipowasili Mkoani hapo na kupokelewa na viongozi mbalimbali baada ya kuteuliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutokea Mkoa wa Morogoro, alisema viongozi waache kasumba ya kuwazuia watumishi kuongea na viongozii wao kwani imekuwepo dhana ya baadhi ya viongozi kuchukia iwapo mtumishi wa chini yake atapata nafasi ya kuongea na kiongozi wa juu.
“kuna baadhi yetu mtumishi akitaka kuonana na Mkuu wa Mkoa ama Mkuu wa Wilaya ananuna sasa una nuna nini unajua mtumishi anaenda kuongea nini labda anakwenda kuongea nae mambo binafsi au vinginevyo lakini mnachukia jamani sisi wote ni viongozi tujenge utamaduni wa kusaidiana na kusikilizana katika kazi ili tuweze kuleta maendeleo katika Mkoa wetu” alisema Shigela.
“nafarijika kuja kufanya kazi nanyi wanageita kwakua Mkoa wetu una agenda mkoa wetu una watu wanaojituma kutafuta maendeleo kwa bidii name na viongozi wenzangu tutashirikiana nayi kuhakikisha maendeleo yanapatikana kikubwa niendelee kusisitiza mshikamano,upendo na ushirikiano hiyo ndio iwe nguzo yetu itakayotuvusha” alisema Shigella.
MKUU WA MKOA AKISALIMIANA NA VIONGOZI ALIPOWASILI OFISINI
Akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Geita Kaimu katibu tawala wa Mkoa wa Geita Herman Matemu alisema Mkoa w Geita ni salama kutokana na kudhibiti matukio ya uhalifu kuanzia ngazi ya mitaa hivyo kuufanya Mkoa kuendelea kuwa shwari,alisema Mkoa una ratibu na kusimamia shughuli zote za maendeleo zinazoendelea kufanyika ambapo miradi mingi iko katika hatua za ukamilishaji.
“Mkoa unasimamia na kuratibu shughuli zote za maendeleo zinazofanyika ambpo miradi mbalimbali ipo katika hatua zinazoridhisha ikiwemo ujenzi wa uwanja wa mpira,ujenzi wa nyumba ya makazi ya Mkuu wa Mkoa ujenzi wa ofisi na nyumba za makazi za wakuu wa Wilaya Mbongwe na Nyang’hwale”alisema Matemu.
MKUU WA MKOA WA GEITA MARTINE SHIGELLA AKIWASALIMIA BAADHI YA VIONGOZINaye Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Saidi Mkumba alisema wakuu wa Wilaya za Geita kwa pamoja wanaahidi kutoa ushirikiano kwa kila kitakachohitajika kwani wao wanamfahamu Shigella kama mtendaji na kwamba wako tayari kufanya kazi ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Geita.
“sisi kama wasaidizi wako tunakuahidi kuwa tutafanya kazi ya kuleta maendeleo kazi ya kutatua kero za wananchi na tunaamini sasa tunaenda kujenga misingi imara ya utendaji kazi na itakua kazi ya muendelezo aliyoiacha mama yetu Rosemary Senyamule aliyokua akiifanya kwa kushirikiana nasi” alisema Mkumba.
VIONGOZI MBALIMBALI MKOA WA GEITA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA GEITA MARTINE SHIGELLA(hayupo pichani) ALIPOWASILI OFISI ZA MKUU WA MKOA WA GEITAMWISHO.
0 Maoni