Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jeneral Charles Mbuge akiongea na baraza la UVCCM Kagera
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la umoja wa vijana uvccm
Mkoani Kagera katika tathimini ya maendelo kwa kipindi cha miaka
mitano ndani ya chama hicho Mkuu wa Mkoa amesema kuwa
kuna baadhi ya wanasiasa wasiopenda maendeleo wamekuwa wakiwatumia baadhi ya vijana kwa masilahi yao binafsi na kushindwa kulitanguliza Taifa, wanakuwa wawanasiasa uchwala waliopitwa na wakati badala yake amewataka vijana wabadilike wawe mfano mzuri wa watangulize maslahi ya Nchi Mbele kuliko fedha za wanasiasa hao .
Awali akiwasilisha changamoto na maombi ya Baraza hilo kaimu
mwenyekiti Bi. Sophia Busunge ameiomba serikali kuwakumbuka
kwa kuwapatia vitendea kazi zikiwemo mashine za kufyatua
matofari,zana za uvuvi,mizinga ya kufugia nyuki kilingana na uhitaji
wa kila wilaya pamoja ana kuwaanzishia viwanda vidogo vidigo ili i
werahisi wao kama jumuiya kuweza kakabiliana na hali ya
Marejesha ya mikopo na kupunza hali ya vijana kukimbia na mikopo
kwa sasa wanahaidi kukaa katika eneo moja la kufanya kazi.
0 Maoni