Picha ya Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Willson Sakulo.

MISSENYI

Katika kuboresha elimu na kuongeza ufaulu mashuleni Serikali ya awamu ya sita imetoa na kugawa vitabu 19,364 Vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 36.5 katika shule za sekondari 22  Wilayani Missenyi Mkoani Kagera ili kutatua tatizo la uhaba wa vitabu vya masomo mashuleni.

Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo  kwenye Halmshauri Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Willson Sakulo amesema kuwa serikali imefaya hivyo ili kuongeza nyenzo kwa wanafunzi kuelimika  na kuwataka walimu vitabu hivyo walivyo pewa wasivitunze makabatini bali vitumike kuleta tija kwa wanafunzi ndani ya wilaya hiyo.

 “ hivyo sita vumilia kusikia vitabu hivyo vimehujumiwa kwa namna yoyote ile pamoja na kuuzwa katika taasisi binafsi, hivi vitabu vimegawiwa katika shule za serikali sasa vitakapo onekana katika shule binafsi inamaana ni hujuma muhusika atakaye kuwa amefanya hivyo atachukuliwa hatua, naomba mlizingatie hili amesema Kanali Wisson Sakulo.


Picha ya Afisa Elimu Sekondari Wilaya Missenyi Baraka Maya.

Afisa Elimu sekondari wilaya Missenyi Mbaraka Maya amesema kuwa vitabu hivyo vitasaidia kuongeza ufaulu mashuleni ambapo wilaya hiyo awali kwa shule za sekondari ilikuwa na vitabu 15 elfu katika masomo yote na kwa sasa idara ya elimu imeshaweka mikakati mbalimbali ya kuinua taaluma hiyo, kwa kukaa vikao na wakuu wa shule pamoja na walimu kuinua kiwango cha taaluma likiwemo la kuunda makundi ya kusoma kwa wanafunzi na kubaini wanaofanya vibaya na kuwatengenezea mazingira ya kuibuka kwa mwaka huu ambapo Wilaya imeweka malengo ya kufanya vizuri kuliko miaka iliyopita.


Picha Mkuu wa Wilaya akikabidhi kitabu Mkuu wa Shule Kyaka kwa niaba ya Wakuu wa shule Missenyi.

Kwa upande wao Baadhi ya wakuu wa shule walio kuzungumza na kituo hiki Mesi Mlema na Manyosisie Molice wamesema  kwa sasa wameishukuru serikali kwa kuongezea vitabu hivi kazi yao ni kwenda kuongeza bidii na kuongeza uelewa kwa wanafunzi na ufaulu.

Mthibiti Ubora Wilaya missenyi Bulenga Mrefu ameeleza kuwa ugawaji wa vitabu hivi litaongeza kujifunza wanafunzi na kufundisha kwa walimu kwa shule za serikali na kuleta tija ambapo kuhadi kusimamia vitabu hivyo vinatumika kwa matumizi na wakati uliosahihi ili kila mwanafunzi afurahiye fursa iliyotolewa na serikali katika ziara yake kwa shule atakazo tembelea.