Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kagera mhandisi Godlove Mathayo.
KAGERA
Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Kagera wameliomba Shirika la Umeme nchini Tanesco kutekeleza kwa umakini mfumo mpya wa kuwaunganishia huduma za umeme majumbani mwao kwa kutumia simu na Kompyuta maarufu kama Ni- Konekt ili kuwawezesha kuondokana na kero ya kutapeliwa fedha zao na vishoka, na kuishia kutopata huduma hiyo kama wateja.
Wakizungumza na The Profile Tv Emmanuel Kato,Rosemary Peter na Nestory Twigwera wakati wa uzinduzi wa mfumo huo wa Ni-konekt uliofanyika katika manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera wananchi hao wamesema kuwa mbali na kutapeliwa na vishoka pia mfumo wa zamani umekuwa ukisababisha kupoteza muda na gharama kubwa katika ufuatiliaji wa kutumia siku nzima pasipokupata mafanikio na kuwa huu mfumo inaonekana utaleta tija na utaondoa usumbufu kwa wateja na mambo ya rushwa na ya kuzungushwa yatakwisha, utashawishi watu wengi kuwa na mwamko kuomba kuunganishiwa umeme.
Baadhi ya wateja wa Tanesco Mkoa wa Kagera
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kagera mhandisi Godlove Mathayo amesema kupita mfumo huo kufikia juni sita walikuwa wamepokea maombi 61 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo wakihitaji kufungiwa huduma ya umeme na kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa na mwitikio mkubwa tofauti na awali ambapo kulikuwa na malalamiko mengi ya kupoteza mafaili na kwamba jambo hilo halitakuwepo kwa sababu kumbukumbu zote zitawekwa kwenye mfumo wa internet aidha amesema faida nyingine ni kuondokana na vishoka ambao huwalaghai wateja.
Jengo la Tanesco Mkoa wa Kagera
Mhandisi Edwin Edward amezungumza na The Profle tv kuhusu mfumo mpya ili kupunguza adha kwa wateja amesema Kuna baadhi ya wateja walikuwa wanaleta makaratasi ya kujaza ya ukandarasi, wengine wakienda wakakutana na changamoto wanayatelekeza kwao na hawarudi, lakini sasa wataepuka kujaza hayo makaratasi na kwamba wanatumia kompyuta na kutuma data za wateja, kwa haraka pamoja na kujibiwa kwa wakati
0 Maoni