Picha ya Mkuu wa Wilaya Muleba Toba Nguvila.
KAGERA
Baadhi ya
wafanyabiashara Nchi za jumuiya Afrika Mashariki wameiomba serikali ya Tanzania
kuwaondolea vikwazo wanavyo kutana navyo katika mipaka ya nchi hiyo jambo ambalo
linawapatia wakati mgumu kwenye ufanyaji wa kazi nchini.
Wakitoa kilio
chao Baadhi ya Wafanyabiashara wa Nchi ya Tanzania,Burundi,Uganda na Congo
katika maonyesho ya jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea Manispaa ya
Bukoba Mkoani Kagera kwa Mkuu wa wilaya Muleba Toba Nguvila aliyefungua
maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jeneral Charles Mbuge ambapo
wasema mizigo yao inashikiliwa mara kwa mara nakupelekea kukaa kwa zaidi ya
siku tatu bila kufanya biashara jambo ambalo linapelekea mabalozi wa nchi hizo
kwenda kuzungumza na TRA waweze kufunguliwa.
Picha ya Mratibu wa maonesho ya Afrika Mashariki Mkoani Kagera William Ruta.
Mratibu wa
maonesho hayo William Ruta amesema maonesho yameanza tangu Tarehe 15 mwezi juni
mwaka huu na mategemeo yao kama waandaaji yamevuka malengo ambapo washiriki kutoka
mikoa mbalimbali nchini wamejitokeza aidha maonesho hayo
yamehudhuriwa na nchi jirani za Burundi,Congo na Uganda na kutumia nafasi hiyo
kuishuru serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikino wa
Afrika Mashariki kwa kuwapata vibali washiriki.
kwa upande
wake Mkuu wa wiliya Muleba Toba Nguvila ambaye alikuwa mgeni rasimi katika
kufungua Maonesho hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jeneral Charles
Mbuge amewata mamlaka ya mapato TRA Kuwaondolea vikwazo wafanyabiashara katika
mipaka na kusema kuwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka yote
nchini Tanzania pamoja na kuinganisha na nchi jirani ndani ya Afrika Mashariki
kwa vikwazo vilivyo ongelewa hapendi vitokee Mkoani Kagera.
Picha Mbalimbali za Baadhi ya washiriki katika Maonesho ya Afrika Mashariki.
0 Maoni