Picha ya Naibu katibu Mkuu Tamisemi sekta ya Afya Dkt. Grece Magembe wakati akizungumz na watumiashi wa Afya Mkoani Kagera.
“Natoa muda wa wiki Mbili wakurugenzi leteni hizo Taarifa ili tuweze kuziba hizo nafasi hakuna kusubiriana umepata bahati ya kupata ajira nenda kituo chako cha kuripoti kama ulivyo elekezwa fail ya kufanya hivyo nafasi yoko tutaiziba kwa kumpatia mtumishi mwingine wananchi wapo wanakusubiri kupata huduma kwa hiyo hatuna muda wa kusubiriana wala kubembelezana.
Naibu katibu Mkuu Tamisemi sekta ya Afya Dr. Grece Magembe ametoa Muda wa Wiki Mbili kwa Watumishi wote waliopata nafasi ya ajira serikalini kuripoti kwa wakati katika Vituo vyao walivyopangwa na kusema kuwa atakayeshindwa kufika ndani ya Muda huo nafasi yake atapewa mtu mwingine.
Picha Baadhi watumishi wa mbalimbali wa serikali Mkoani Kagera.
0 Maoni