GEITA KUVUTIA WAWEKEZAJI
NA ROSE MWEKO, GEITA.
MKUU wa Mkoa wa Geita Bi Rosemary Senyamule amesema ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchi ya Dubai imezaa matunda ambapo tayari wawekezaji kadhaa wameonyesha nia ya kuwekeza Mkoa wa Geita jambo ambalo litaleta neema kwa wananchi na Serikali kwa ujumla.
Bi Senyamule aliyasema hayo mjini Geita katika kikao kazi na viongozi wa Mkoa na wakuu wa idara mbalimbali alisema hatimaye Mkoa wa Geita umepata watu walioonyesha nia ya kuwekeza katika sekta mbalimbali hivyokuwataka wakuu wa idara kuwa tayari katika kuandaa miundombinu wezeshi itakayowashawishi wawekezaji.
“tunapaswa kuwa tayari kujiandaa na wawekezaji ambao watafika hapa hivi karibuni katika ziara ya Mh Rais ambayo name nilibahatika kuwawakilisha tulikwenda na mikakati ya kuwavutia wawekezaji na sasa wameonyesha nia ya kuja kuwekeza kwetu, sasa kuwavutia tu si kigezo cha kupata wawekezaji bali ni katika kuandaa mazingira wezeshi yatakayowafanya wavutiwe kukaa nasi na si kwenda sehemu nyingine niwaombe wakurugenzi na watendaji wa Halmashauri kuainisha na kutenga maeneo yaliyotayari kutumika kwa uwekezaji pia huduma muhimu za maji,umeme na barabara viandaliwe” alisema Bi Senyamule.
Alisema juhudi za Mh Rais zimezaa matunda hivyo watendaji wanapaswa kutokumuangusha kwa kuandaa miundombinu wezeshi kwani wawekezaji watakaofika Geita wako tayari kushirikiana na Serikali ya Mkoa kuifanya Geita kuwa na maendeleo kupitia sekta ya madini,kilimo na uvuvi.
Aidha Bi Senyamule amewataka viongozi wa Mkoa kuhakikisha wanakuwa na uwazi katika kutekeleza miradi mbalimbali katika jamii ili kuwafanya wananchi waweze kuwajibika katika kuilinda na kuiendeleza, alisema miradi mingi ipo kwa ajili ya wananchi lakini mara nyingi inatekelezwa bila ushirikishwaji wa wananchi jambo ambalo haliwapi hamasa wananchi kuona kuwa hiyo ni miradi yao na hivyo kutoilinda.
“tunajua kabisa halmashauri zetu hazina wataalamu wa kutosha na miradi tuliyonay ni mingi kwa hivyo nashauri tuwashirikishe wananchi huko vijijini, huko vijjini tuna mafundi na wengine wanaujuzi kwa uzoefu tu kama tutawashirikisha watatusaidia sana katika kukamilisha miradi yetu kuliko kutojua nini kinafanyika hapo watakapoelimishwa naamini watajitoa kwa moyo na hilo ndilo lengo la Serikali” alisema Bi Senyamule.
“na nyie mnajua wananchi ni wazuri sana kwa usimamizi wakijua kinachotakiwa hivyo naagiza kila Halmashauri kubandika miradi yote inayofanyika mapato na matumizi katika mbao za matangazo hii itasaidia kuwa na usimamizi utakaotusaidia kupata matokeo mazuri ya miradi tnayoitekeleza kule vijijini wapo wataalamu ambao hawajasomea lakini wanajua baadhi ya kazi na kwao itakua rahisi kuimamia” alisema Bi Senyamule.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Henry Mwaibambe ameitaka Seriksli inapoandaa maeneo ya uwekezaji iwezekuwashirikisha na vyombo vya usalama ili kuhakikisha wawekezaji wanakuwa salama wao na mali zao nah ii itasaidia kuepusha migogoro itakayoiharibia sifa Tanzania.
“mara nyingi hata mnapopanga kuanzisha Mkoa mpya Polisi mnaisahau,mnapopanga kuanzisha maeneo mapya ya kiutawala vyombo vya ulinzi mnavisahau naomba niwaambie ndugu zangu wenzetu wa huko nje mnapowaambia hii ni nchi ya amani wanajua ni amani muda wote sasa hakikisheni mnapoandaa miundombinu ya uwekezaji muandae na maeneo ya vyombo vya usalama ili kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa”alisema Mwaibambe.
Mwisho.
0 Maoni