MKUU WA MKOA WA GEITA BI ROSEMARY SENYAMULE AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI KATIKA UZINDUZI WA MAONESHO YA TATU YA WAFANYABIASHARA MAARUFU KAMA FAHARI YA GEITA 

NA ROSE MWEKO, GEITA.

MAONESHO ya tatu ya biashara Mkoani Geita maarufu kama FAHARI YA GEITA yanayosimamiwa na African Creative yamefunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Geita Bi Rosemary Senyamule lengo ikiwa kuwawezesha wafanyabiashara kutafuta mawasiliano na mahusiano ya kibiashara baina ya wafanyabiashara wa ndai na nje ya nchi.

Akizungumza na wafanyabiashara na washiriki wa maonesho hayo Mkuu wa Mkoa alisema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuwa jukwaa la kuwakutanisha wafanyabiashara na wajasiliamali na taasisi za kifedha na taasisi za umma ili kuweza kutengeneza mtandao wa kibiashara na hatimaye kukuza biashara.

Bi Senyamule alisema kazi ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wanakaa kwa amani na utulivu ili kuwatengenezea mazingira mazuri wananchi kujitafutia kipato na kujiletea maendeleo, Serikali ya Mkoa wa Geita  imewaandalia mazingira mazuri ya ulinzi na usalama wa bidhaa zao  wafanyabiashara walioshiriki katika katika maonyesho hayo.

“sisi kama Serikali tunaungana na waandaaji na wasimamizi wa maonyesho haya kuhakikisha usalama wao na bidhaa zao na hiyo ndio kazi kuu ya Serikali kutengeneza mazingira wezeshi kwa wananchi na ndio maana ninahamasisha taasisi za kihuduma zilizoko chini ya Serikali kujitokeza kushiriki maonyesho haya ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi na sehemu moja, kwani ninaambiwa taasisi zilizojitokeza mpaka sasa ni kumi na sita”alisema Senyamule.

“Aidha tunaendelea kualika sekta binafsi kuja kuwekeza katika Mkoa wetu wa Geita kwani Geita ina ardhi nzuri yenye rutuba pia tuna ziwa Victoria ambayo inaweza kutumik kwa uvuvi mkubwa wa kibiashara pia Mkoa wetu wa Geita una madini ya dhahabu na hifadhi  ya Burigi-Chato kwa kutambua fursa hizo Mkoa umeandaa kituo cha uwekezaji ili kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara watakaokuwa na nia ya kuwekeza Mkoani kwetu nitoe wito kwa wananchi kujiandaa kwa ajili ya kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji watakaofika Mkoani hapa kutafuta fursa za uwekezaji ili watukute tukiwa tayari” alisema Senyamule.

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa African Creative Rafael Siyantemi alisema maonesho haya yameandaliwa na African Creative kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo Sido na TCCIA ambapo imewashirikisha washiriki miambili kumi na moja na taasisi za umma kumi na sita aidha taasisi za huduma za serikali na zile za binafsi zimeshiriki katika maonyesho haya na zinatoa huduma kwa haraka katika eneo moja hivyo kuwakaribisha wananchi kutembelea viwanja vya kalangalala yanapofanyika maonesho hayo.

“Mheshimiwa Mgeni Rasmi sekta binafsi inaendelea kukushukuru wewe na ofisi yako kwa kushirikiana kwa karibu nasi aidha shirika la kuhudumia viwanda vidogo sido ipo katika maonesho haya na kutoa huduma ya ushauri kwa wajasiliamali na wasindikaji wa bidhaa mbalimbali walioshiriki katika maonesho haya aidha inatoa wito kwa wajasiliamali kufika katika banda la sido kupata ushauri wa kitaalamu” alisema Siyantemi.

“Aidha tunaomba ofisi yako iendelee kutoa ushirikiano pindi tunapohitaji aidha iendelee kutuonyesha fursa  pindi zinapojitokeza ili wafanyabiashara na wajasiliamali waweze kuzitumia na hatimaye kunufaika nazo nah ii itasaidia kukuza uchumi wa wananchi wa Geita” alisema Siyantemi.

MWISHO.