Waandishi wa habari wanawake wacheza mechi ya kirafiki na waheshimiwa wabunge wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambapo timu ya wabunge yaibuka kidedea baada ya mheshimiwa spika Tulia kuibuka kinara kwa kuipa timu yao magori murua 

Mechi hiyo yafanyika baada ya waandishi wahabari wanawake takribani 21 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania kufika Bungeni hapo wakiwa Ni wageni wa Spika.


Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete ya Wanawake ikiongozwa na Spika Dkt. Tulia Ackson, imeichalaza timu ya Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania kwa magoli 31-10 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

 Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ameipongeza timu ya Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania kwa uthubutu wa kuweza kucheza licha ya kuonekana kutokuwa na mazoezi Huku akieleza Siri ya mafanikio Yao .

 Pia amesema Chama cha Netball Tanzania kimepata uongozi mpya,anaamini kitakuja na mkakati mzuri wa kuendeleza mchezo huo ili uende vizuri kama ilivyo kwa mchezo wa mpira wa miguu hivyo wale wanaopenda kucheza waanze wakiwa wadogo na waendelee kuweka bidii huku kwa upande wao wataendelea kutoa ushirikiano.

 Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji walikuwa na haya ya kusemaHata hivyo waandishi wa habari Wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini wamefanya ziara ya siku mbili jijini Dodoma ambapo walipata fursa ya kuhudhuria Bunge na kujifunza namna shughuli za Bunge zinavyofanyika pamoja na kucheza mchezo huo wa kirafiki wa mpira wa pete.