
Waandishi waliowasiliana na blogu ya Francis Godwin, Moes Ng'wati na Brandy Nelson wanaripoti kuwa tukio la kuteketea kwa soko limetokea leo asubuhi majira saa 3:10 na moto huo bado unaendelea kuwaka
Baada ya eneo la katikati la soko kulipuka na kuanza kuwaka moto huku tayari wafanyabiashara wakiwa wameshafungua maduka na vibanda vyao wakiendelea na biashara, ndipo waliposhuhudia moto huo. Walioshuhudia tukio hilo wanasema wafanyabiashara walianza harakati za kuuzima moto huo bila mafanikio huku wengine wakijitahidi kuokoa mali zao kwa ziondoa eneo la soko, “kwa kweli moto ni mkubwa na hatujui chanzo chake nini kwani ghafla tumeona moto ukiwaka eneo la soko upande wa katikatika wa soko hilo hivyo kila mtu anashangaa ulikoanzia moto huu” alisema mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Francis James. Alisema kuwa magari ya zimamoto ya halmashauri ya jiji la Mbeya yamefika eneo la tukio lakini yameshindwa kuuzima moto huo baada ya kuonesha kuongezeka kwa kasi kuwa mkubwa na badala yake wananchi kufanya juhudi ya kuokoa mali zao, “Kwa sasa tayari jeshi la polisi limefika hapa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kuokoa mali zao ikiwa ni pamoja na kuzuia vibaka kuiba mali za watu kwani hali ni mbaya wafanyabiashara na wananchi wengi wamechanginikiwa kutokana na magari hayo kushindwa kuzima moto huo”alisema |
0 Maoni